Tolu Bally
Tolulope Bally kitaaluma anajulikana kama Tolu Bally (alizaliwa 2 Oktoba 1988) ni mtendaji mkuu, mfanyabiashara, na mjasiriamali wa mitindo wa nchini Nigeria.[1][2] Ni mwanzilishi na mkurugenzi wa 2207bytbally, chapa ya mitindo nchini Nigeria iliyobobea katika mavazi ya kike..[3][4]
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Tolulope alizaliwa 2 Oktoba 1988 katika familia ya Mr & Mrs Bally kama mtoto wa mwisho. Ana asili ya Nupe na Yoruba kutoka Jimbo la Ondo, Nigeria. Alisoma katika Chuo cha Newham, Uingereza kabla ya kujiunga na Chuo kikuu cha East London, Uingereza ambako alihitimu na shahada ya awali katika masomo ya Saikolojia.[5][6]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Bally alihamia London, Uingereza ili kuendeleza elimu yake. Akiwa London, alijishughulisha na biashara ya uuzaji wa nguo na ndipo alipogundua mapenzi yake katika mitindo ya nguo.[7] Baada ya masomo nchini Uingereza alirudi Nigeria kwa ajili ya kuendeleza ujuzi wake wa mitindo ya nguo.[8][9]
Mnamo 1 Novemba 2016, alianza rasmi kazi yake ya mitindo.[10] Aliita chapa yake ya mitindo "2207bytbally", chapa inayohusika na mavazi ya wanawake.[11]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Iwalaiye, Temi (2021-09-25). "Beauty Inspiration: Why Tolu Bally is the ultimate black barbie". Pulse Nigeria (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-09-06.
- ↑ Iwalaiye, Temi (2023-03-22). "10 influential women in Nigeria's fashion scene". Pulse Nigeria (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-09-06.
- ↑ "Tolu Bally's 2207byTbally plans anniversary treats". The Nation Newspaper.
- ↑ "Top 10 Nigerian Designers Redefining Owambe Outfits" (kwa American English). 2022-06-20. Iliwekwa mnamo 2023-09-06.
- ↑ "Fashion Designer, Tolu Bally Is The Definition Of A Black Beauty In Spades". koko.ng (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2022-09-24. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-09-06. Iliwekwa mnamo 2023-09-06.
- ↑ "Tolu Bally reveals her quest for perfection - THISDAYLIVE". www.thisdaylive.com. Iliwekwa mnamo 2023-09-06.
- ↑ Dokubo, Titi (2022-06-29). "29 Black Female Designers You Should Know". Style Rave (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-09-06.
- ↑ Iwalaiye, Temi (2022-12-02). "Who wore it best? Fashionistas take on a 2207byTbally black gown". Pulse Nigeria. Iliwekwa mnamo 2023-09-06.
- ↑ Henshaw, Nelly (2020-11-15). "Tolu Bally, the Ace Designer Ruling the Fashion Scene with Every Stitch". Svelte Magazine (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-09-06.
- ↑ Mag, Lagos (2023-05-06). "Fashion Pick of The Week: Tolu Bally Creates And Sets Trends With Her Fashion Statements". The Lagos Magazine (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-09-06.
- ↑ Yaakugh, Kumashe (2022-11-29). "Tolu Bally's Dress Recreation Spotted on Osas Ighodaro Sparks Mixed Reactions". Legit.ng - Nigeria news. (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-09-06.