Tipaza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tipaza (mwanzoni ilifahamika kama Tefessedt lugha ya Chenoua-Berber: Bazar, ⴱⴰⵣⴰⵔ) ni eneo kuu la Jimbo la Tipaza, Algeria. Wakati wa utawala wa Kiroma, ilifahamika kwa jina la Tipasa. Mji huo wa kisasa ulianzishwa mnamo mwaka 1857, na unatambulika zaidi kwa uwepo wa mabaki ya majengo ya kale pamoja na mchanga wa fukwe za bahari.


Historia[hariri | hariri chanzo]

Historia ya Kale[hariri | hariri chanzo]

Tipasa, kama ilivyokua ikifahamika, ilikua sehemu ya biashara za watu wa jamii ya Punic wakati wa utawala wa Roma. Baadaye iligeuzwa na kuwa koloni la kivita chini ya utawala wa Kiroma ikiongozwa na Mfalme wa kipindi hicho Claudiu kwa lengo la kuchukua utawala wa falme ya Mauritania.[1]

Baadaye ikageuzwa kuwa manispaa na kupewa jina la Colonia Aelia Tipasensis, ambayo ilifikia idadi ya wakazi 20,000 katika karne ya nne, na hii ni kwa mujibu wa Stéphane Gsell.

Mji huu una umuhimu mkubwa kama eneo lililochangia kukuwa kwa dini ya kikristo wakati wa kuishia kwa utawala wa Kirumi.

Tipasa iliharibiwa na ..Vandals.. miaka ya 430, lakini iliundwa upya wakati wa utawala wa Byzantine karne moja baadaye. Mwishoni mwa karne ya saba, mji huo uliharibiwa na majeshi ya ..Umayyad Caliphate.. na kubakia magofu.[2]

Katika karne ya kumi na tisa, mji huo uliundwa tena, wakati huo ukawa na wakazi wapatao 30,000. Kwa sasa mji huu una mchango mkubwa katika sekta ya utalii nchini Algeria hasahasa kutokana na magofu ya Tipas.

Kizazi cha Sasa[hariri | hariri chanzo]

Karibu na Tipaza, shirika la Tipaza Longwave Transmitter hurusha matangazo kwa lugha ya kifaransa kutoka shirika la utangazaji la Algeria. Masafa marefu ya matangazo hayo yaliweza kusikika mpaka bara la Ulaya.

Mji huo na maeneo yanayoizunguka ni makazi ya kabila lenye watu wengi zaidi nchini Algeria la Chenouas.

Kituo cha redio cha Tipaza chenye masafa ya 252 kHz ilishindwa kufanya kazi tangu Machi 17, 2014, lakini kwa sasa inarusha matangazo yake kupitia masafa ya 252 kHz.[3]

Kichanja cha picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Unesco-page
  2. Toutain, Jules (1891). "Fouilles de M. Gsell à Tipasa : Basilique de Sainte Salsa". Mélanges d'archéologie et d'histoire. 11 (1): 179–185. doi:10.3406/mefr.1891.6684.
  3. see [1] - tuned to 252khz, as of 2015 Sept. 22

Viunga vya nje[hariri | hariri chanzo]

Tipaza travel guide kutoka Wikisafiri

Wikimedia Commons ina media kuhusu: