Nenda kwa yaliyomo

Tinga Chan, Tinga Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tinga Chan, Tinga Tanzania ni kampeni maalumu kwa ajili ya CHAN 2025.[1] Kampeni ya Tinga Chan, Tinga Tanzania ni mpango maalumu uliobuniwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kwa lengo la kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya utalii kupitia mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), ambayo yamepangwa kufanyika kuanzia tarehe 2 Agosti hadi tarehe 30 Agosti, mwaka 2025.[2]

Uzinduzi wa Kampeni

[hariri | hariri chanzo]

Kampeni hii ilizinduliwa rasmi mnamo tarehe 31 Julai 2025, katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Bw. Ephraim Mafuru, alieleza kuwa lengo kuu la kampeni ni kutumia fursa ya CHAN 2025 kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ndani na nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Mafuru, mataifa 19 ya Afrika yatashiriki katika mashindano hayo. Aidha, Watanzania kutoka mikoa ya Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na Dar es Salaam wataweza kutazama mechi moja kwa moja kupitia maeneo maalum ya kuoneshea michezo.

Wito kwa Umma na Maandalizi

[hariri | hariri chanzo]

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Bw. Rodney Thadeus, alithibitisha kuwa maandalizi ya CHAN 2025 yamekamilika kikamilifu, na akaeleza kuwa mashindano hayo ni zaidi ya tukio la michezo.

Umuhimu wa Kampeni

[hariri | hariri chanzo]

Kampeni ya Tinga Chan, Tinga Tanzania inatarajiwa kuongeza mwamko wa kitaifa kuhusu utalii, kuhamasisha ushiriki wa jamii katika michezo, na kuimarisha taswira ya Tanzania kimataifa kupitia ushiriki wake katika mashindano ya CHAN.

Usaidizi na Ushiriki wa CHAN 2025

[hariri | hariri chanzo]

Mashindano ya CHAN 2024 (yanayofanyika mwaka 2025) yalifanyika kwa mara ya kwanza kwa mfumo wa wenyeji watatu, yakisimamiwa na Kenya, Tanzania na Uganda kati ya tarehe 2 Agosti hadi 30 Agosti 2025.Tanzania iliboresha miundombinu yake ikiwemo uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na kufanikisha kuifikisha timu ya Taifa (Taifa Stars) hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hii. Katika hatua ya makundi, Tanzania ilimaliza ikiwa na pointi 10 baada ya kushinda mechi tatu kati ya nne na kuruhusu goli moja pekee, kabla ya kuondolewa na Morocco kwenye robo fainali.[3]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-08-14. Iliwekwa mnamo 2025-07-31.
  2. https://dailynews.co.tz/tanzania-launches-tinga-chan-tinga-tanzania-slogan/
  3. Lunyamadizo Mlyuka (2025-08-22). "Tanzania vs Morocco robo fainali dume Uwanja wa Mkapa" (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2025-09-11.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Tinga Chan, Tinga Tanzania kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.