Timu ya taifa ya kandanda ya Uganda
Timu ya taifa ya kandanda ya Uganda, inayojulikana kama Korongo wa Uganda (The Cranes), inaiwakilisha nchi ya Uganda katika soka la kimataifa. Uwanja wa taifa wa Uganda unafahamika kwa jina la Mandela National Stadium katika mji wa Bweyogerere, nchi ya Uganda. Timu inasimawiwa na Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu vya Uganda (FAFU). Kocha mkuu kwa sasa ni Paul Put, mwenye asili ya Ubelgiji. Kapteni kwa sasa ni Khalid Aucho. Godfrey Walusimbi alicheza mechi nyingi zaidi kwa Korongo wa Uganda (105), na Emmanuel Okwi ni mfungaji bora (28).
Historia
[hariri | hariri chanzo]Korongo wa Uganda ilicheza debi katika tarehe 1 Mei 1926 dhidi ya Kenya, mahasimu wao wa Afrika Mashariki, ambayo ilimalizika kwa suluhu ya 1-1. Katika 1962, Korongo wa Uganda ilifanya dabi katika Mashindano ya Afrika, mashindano matatu, ambayo ilikuwa na timu nne tu. Korongo wa Uganda ilipoteza mecha dhidi Misri 2-1, na ilipoteza mecha ya nafasi ya tatu dhidi Tunisia 3-0. Timu hii imefuzu Mashindano ya Afrika mara nane, na imewahi kumaliza nafasi ya pili katika Mashindano ya Afrika ya 1978. Uganda, Kenya, na Tanzania watakuwa wenyeji wa Mashindano ya Afrika ya mwaka 2027. Timu ya Taifa ya Uganda imekuwa ikishindana katika Mashindano ya CECAFA kutoka mwaka 1926 mpaka sasa. Wao wameshinda mashindano mara arobaini, ambayo ni mataji mengi zaidi ya taifa lolote. Korongo wa Uganda haijawahi kufuzu kwa Kombe la Dunia, hata hivyo. Katika mwaka 2016, timu ilikuwa “Timu Bora ya Afrika ya Mwaka”.
Mechi nyingi zaidi
[hariri | hariri chanzo]Daraja | Mchezaji | Mechi | Magoli | Kazi |
---|---|---|---|---|
1 | Godfrey Walusimbi | 105 | 3 | 2009-2019 |
2 | Emmanuel Okwi | 95 | 28 | 2009-2023 |
3 | Simeon Masaba | 88 | 6 | 2002-2013 |
4 | Tony Mawejje | 86 | 8 | 2003-2018 |
5 | Denis Onayngo | 82 | 0 | 2005-2021 |
6 | Hassan Wasswa | 81 | 0 | 2006-2019 |
7 | Farouk Miya | 79 | 23 | 2014-sasa |
8 | Khalid Aucho | 76 | 2 | 2013-sasa |
9 | Andrew Mwesigwa | 75 | 7 | 2003-2014 |
10 | Geoffrey Massa | 72 | 22 | 2005-2017 |
Kikosi cha sasa
[hariri | hariri chanzo]Wachezaji 26 walichaguliwa kuiwakilisha Uganda katika mchezo wa kufuzu Mashindano ya Afrika dhidi Msumbiji na Guinea tarehe 20 na 25 mwezi Machi mwaka 2025.
Nafasi | Mchezaji | Tarehe ya Kuzaliwa | Mechi | Magoli | Klabu |
GK | Ismail Watenga | 15 Mei 1995 | 35 | 0 | Lamontville Golden Arrows |
GK | Nafian Alionzi | 1 Machi 1996 | 6 | 0 | Defence Force |
GK | Joel Mutakubwa | 17 Julai 1995 | 3 | 0 | BUL |
| |||||
DF | Isaac Muleme | 10 Oktoba 1992 | 52 | 0 | Viktoria Žižkov |
DF | Timothy Awany | 6 Agosti 1996 | 45 | 0 | Ashdod |
DF | Aziz Kayondo | 6 Oktoba 2002 | 26 | 2 | Slovan Liberec |
DF | Bevis Mugabi | 1 Mei 1995 | 26 | 1 | Anorthosis Famagusta |
DF | Gavin Kizito | 14 Januari 2002 | 12 | 0 | KCCA |
DF | Elvis Bwomono | 29 Novemba 1998 | 10 | 0 | St Mirren |
DF | Toby Sibbick | 23 Mai 1999 | 1 | 0 | Wigan Athletic |
DF | Rogers Torach | 23 Juni 2003 | 1 | 0 | Vipers |
| |||||
MF | Khalid Aucho © | 8 Agosti 1993 | 76 | 2 | Young Africans |
MF | Allan Okello | 4 Julai 2000 | 28 | 3 | Vipers |
MF | Travis Mutyaba | 7 Agosti 2005 | 23 | 3 | Bordeaux |
MF | Kenneth Semakula | 14 Novemba 2002 | 23 | 0 | Club Africain |
MF | Karim Watambala | 3 Machi 2000 | 14 | 0 | Vipers |
MF | Ssekiganda Ronald | 13 Septemba 1995 | 9 | 1 | Villa |
MF | Enock Ssebaggala | 28 Julai 2000 | 0 | 0 | NEC |
| |||||
FW | Rogers Mato | 20 Oktoba 1998 | 31 | 4 | Vardar Skopje |
FW | Muhammad Shaban | 11 Januari 1998 | 25 | 2 | Al-Anwar Al-Abyar |
FW | Steven Mukwala | 15 Julai 1999 | 21 | 1 | Simba |
FW | Denis Omedi | 13 Juni 1996 | 12 | 2 | APR |
FW | Jude Ssemugabi | 3 Machi 1997 | 4 | 1 | Kitara |
FW | Patrick Kakande | 25 Aprili 2003 | 2 | 0 | Villa |
FW | Hakim Kiwanuka | 11 Septemba 2000 | 2 | 0 | APR |
FW | Calvin Kabuye | 28 Machi 2003 | 1 | 0 | Mjällby |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- https://www.fufa.co.ug
- https://www.national-football-teams.com/country/195/2025/Uganda.html
- https://www.worldfootball.net/teams/uganda-team/21
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Timu ya taifa ya kandanda ya Uganda kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |