Tikvah Alper
Tikvah Alper (22 Januari 1909 - 2 Februari 1995) alikuwa mtaalamu bingwa wa mionzi, ambaye alipata mafunzo kama mwanafizikia. [1] Katikati ya mipango na uvumbuzi mwingine mwingi, alikuwemo kati ya wa kwanza kupata uthibitisho unaoonyesha kwamba wakala wa kuambukiza kwenye scrapie hauna asidi ya kiini : ugunduzi ambao ulikuwa wa msingi kwenye kuelewa maendeleo ya nadharia ya prioni . Alikuwa mkurugenzi wa Kitengo cha Majaribio cha Radiopatholojia ya MRC, Hospitali ya Hammersmith, London, Uingereza, 1962-1974.
Maisha ya awali na kazi
[hariri | hariri chanzo]Tikvah Alper alizaliwa ndani ya nchi ya Afrika Kusini, mdogo kuliko wote kati ya binti wanne kwenye familia ya wakimbizi wa Kiyahudi kutoka nchi ya Urusi. [2] Akiwa msichana wa shule kwenye Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Durban, watu walimsema kwamba "ni msichana mwenye sifa nzuri zaidi kiakili aliyewahi kuhudhuria shule hiyo", [3] na akahitimu kwa alama ya juu mwaka mmoja mapema. Alimaliza kwa alama ya juu katika fizikia kutoka Chuo Kikuu cha Cape Town mwaka 1929, na bada ya hapo akasoma huko Berlin na mwanafizikia wa nyuklia Lise Meitner mnamo 1930-32, akichapisha karatasi iliyoshinda tuzo [4] kuhusu miale ya delta iliyozalishwa na chembe za alpha mnamo 1933. [5]
Mwaka 1932, alirejea Afrika Kusini ili kuolewa na mtaalamu wa bakteria (baadaye) maarufu Max Sterne, mgunduzi wa chanjo bora zaidi ya mifugo kwa ajili ya kimeta . Aliendelea kutumia jina lake la ukoo katika ndoa miaka yote. Kwa sababu wanawake walioolewa ilikuwa ni marufuku kufanya kazi chuo kikuu enzi hizo, Tikvah na Max walianzisha maabara ya nyumbani mahali walifanya kazi pamoja. Watoto wao, Jonathan na Michael, walizaliwa mwaka 1935 na mwaka 1936. Kuanzia nyakati hizo na kuendelea, Tikvah Alper alichanganya mahitaji ya kuwa mama (Jonathan alizaliwa kiziwi sana), ndoa na kazi. Hizi zilijumuisha vipindi vya kabla na baada ya vita ndani ya nchi Uingereza, ambapo alifanya kazi na mtaalamu wa radiobiolojia waanzilishi, Douglas Lea. [6]
Zaidi ya miaka kumi kutokea mwaka 1937, Tikvah alipata mafunzo tena na kisha pia alihudumu kama mwalimu wa viziwi . Mafunzo yake ya fizikia na ujuzi wake wa kiufundi yalidhuhurishwa kwenye utafiti wake uliochapishwa kuhusu kufanya usemi uonekane, kwa matumizi kwenye mafunzo ya usemi kwa watoto viziwi [7] Alikuwa a afasi ya mkuu wa sehemu ya Biofizikia ya Maabara ya Kitaifa ya Fizikia ya Afrika Kusini mwaka1948.
Kazi ya baadaye
[hariri | hariri chanzo]Japo umaarufu wao wa kisayansi ulizidi kuenea, mwaka 1951, Max Sterne na Tikvah Alper walilazimika kuondoka Afrika Kusini kwa sababu ya upinzani wao wa wazi dhidi ya ubaguzi wa rangi . Tikvah alipata nafasi ya utafiti (isiyolipwa) kwenye Maabara ya Radiobiolojia ya MRC katika Hospitali ya Hammersmith, London, iliyosimamiwa na Hal Gray, ambaye alikuwa ameshakutana naye katika ziara za awali. Hapa, kazi ilikusudia mifumo ya athari za mionzi kwenye biolojia ya seli. Ugumu wa athari za mionzi kwenye aina tofauti za seli, na mwingiliano wao na michakato mingine ya kisaikolojia na kemikali ulianza kuwekewa mipango wakati huu, na kuendelea hadi miaka ya 1950 na 60. Alikuwa na cheo cha mkurugenzi wa Kitengo cha Radiobiolojia kuanzia mnamo 1962 hadi kustaafu kwake mwaka1974. Maandishi yake ya kitamaduni ya Cellular Radiobiolojia yalichapishwa mwaka 1979. Tikvah Alper aliendelea na maisha ya kitaaluma ndani ya kustaafu kwake, na kufikia "hotuba nzuri kwa Jumuiya ya Utafiti wa Mionzi huko Dallas, Marekani akiwa na umri wa miaka 83..". [4] Alifariki dunia Sarisbury, Hampshire, Uingereza, mwaka wa 1995, [8] na aliacha mumewe Max, wanawe Jonathan na Michael, wajukuu sita, na vitukuu watatu.
Jukumu katika utafiti wa scrapie
[hariri | hariri chanzo]Scrapie ni ugonjwa wenye hatari wa kuambukiza wa mfumo wa neva wa kondoo; na ni moja kati ya ya aina ya magonjwa ya prioni yenye uwezo wa kuathiri ng'ombe (BSE) na wanadamu (Kuru, nCJD) . Scrapie ilidhaniwa kusababishwa na 'virusi vya polepole' - ambavyo vinaweza kuchukua miaka kuonyesha kama mabadiliko ya tabia au mwendo. Hadi ilivyofika katikati ya miaka ya 1960, iligundulika kuwa seli zingeweza kujirudia tu kupitia DNA . Utendaji wa mionzi huzuia kujirudia kwa seli kwa 'kuua' DNA. Alper aligundua kuwa mionzi haikuua wakala wa kuambukiza kwenye scrapie, ikidokeza kwamba virusi havina uwezo wa kuwa wakala wa kuambukiza. Wakala wa kuambukiza ilibidi awe mdogo na rahisi zaidi ya DNA (ya virusi). Alper alifanya ugunduzi pia kuwa wakala huyo alibaki akifanya kazi chini ya mwanga wa urujuanimno. DNA haitendi kazi chini ya mwanga wa UV. Badala yake, wakala huyo alikufa kutokana na mwanga akiwa na nyuzi joto 237. nm, urefu wa wimbi maalum kwa kuzuia polysaccharide. Alper na wenzake [9] waliripoti sifa hizi za wakala wa scrapie - ugunduzi ambao ulipokelewa kwa mshangao katika robo nyingi, kwani ulionekana kwenda kinyume na fundisho kuu linaloshikilia kwamba uigaji (na hivyo ukuaji wa ugonjwa na sifa zake za kuambukiza) unaweza kuendelea kupitia DNA pekee. Hata hivyo, baada tu ya matokeo haya ya majaribio yalipokubaliwa, nadharia kadhaa zilitengenezwa ili kuzingatia sifa za kipekee za wakala wa scrapie. Nadharia inayokubalika zaidi leo ni nadharia ya prion, ambayo inadai protini 'rogue' kama chanzo cha kuambukiza. Hata hivyo, Alper hakuweza kukubali kwamba 'mutation' ya protini ndiyo wakala. Kwanza, masomo yake ya mionzi ya UV hayakuonyesha wakala wa protini na, pili, prions zilizotengwa hazikusababisha scrapie. Nadharia zake mwenyewe juu ya wakala zilitengenezwa kwenye miaka ya mwisho ya maisha yake na zilipendekeza hadithi yenye uzito na ngumu zaidi. [10]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Hunter, A (2012). "Radiation biology – An important science". South African Journal of Science. 108 (7/8): 972. doi:10.4102/sajs.v108i7/8.972. hdl:11427/29930.
- ↑ Vogt, Annette B. "Tikvah Alpert 1909-1995". Jewish Women's Archive Encyclopedia. Jewish Women's Archive. Iliwekwa mnamo 17 Desemba 2016.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Hornsey, S; Denekamp, J (1997). "Tikvah Alper: An indomitable Spirit". International Journal of Radiation Biology. 71 (6): 631–42. doi:10.1080/095530097143635. PMID 9246177.
- 1 2 Hornsey, S; Denekamp, J (1997). "Tikvah Alper: An indomitable Spirit". International Journal of Radiation Biology. 71 (6): 631–42. doi:10.1080/095530097143635. PMID 9246177.Hornsey, S; Denekamp, J (1997). "Tikvah Alper: An indomitable Spirit". International Journal of Radiation Biology. 71 (6): 631–42. doi:10.1080/095530097143635. PMID 9246177.
- ↑ Alper, T (1932). "Über die δ-Strahlen und die Beziehung zwischen Reichweite und Geschwindigkeit für langsame Elektronen". Zeitschrift für Physik. 76 (3–4): 172–189. Bibcode:1932ZPhy...76..172A. doi:10.1007/BF01341810. S2CID 122840914.
- ↑ "Lecture by Douglas Lea". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Juni 2012. Iliwekwa mnamo 10 Desemba 2012.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Alper, T.; Zimmerman, H. J. (1939). "A thyraton inflexion indicator for teaching the deaf". Journal of Scientific Instruments. 16 (10): 334–6. Bibcode:1939JScI...16..334S. doi:10.1088/0950-7671/16/10/304.
- ↑ Fowler, J (Aprili 1995). "In memoriam Tikvah Alper 1909-1995". Radiation Research. 142 (1): 110–2. PMID 7899554.
{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Alper, T.; na wenz. (1967). "Does the agent of scrapie replicate without Nucleic Acid?". Nature. 214 (5090): 764–766. Bibcode:1967Natur.214..764A. doi:10.1038/214764a0. PMID 4963878. S2CID 4195902.
- ↑ Alper, T. (Julai 1992). "The infectivity of spongiform encephalopathies: does a modified membrane hypothesis account for lack of immune response?". FEMS Microbiology Letters. 4 (5): 235–242. doi:10.1111/j.1574-6968.1992.tb05000.x. PMID 1355344.
{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)