Nenda kwa yaliyomo

Tigran Keosayan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tigran Edmondovich Keosayan ( Kirusi: Тигран Эдмондович Кеосаян; 4 Januari 196626 Septemba 2025) alikuwa mwongozaji wa filamu, mwigizaji na mtangazaji wa televisheni kutoka Urusi. Alikuwa mshindi wa tuzo za mashindano ya filamu ikiwemo TEFI, Kinotavr, na Window to Europe Film Festival mwaka 2001. [1][2][3][4][5]

Tigran Keosayan alikuwa mtoto wa mwongozaji filamu Edmond Keosayan na mwigizaji Laura Gevorkyan. Alisomea filamu katika taasisi ya VGIK.

Aliwahi kuongoza filamu kama Katyka and Shiz (1992), Poor Sasha (1997), Lily of the Valley Silvery (2005), na Hare Over the Abyss (2006). Pia alifanya video za muziki na kushirikiana na wasanii maarufu wa Urusi.

Keosayan pia alikuwa mtangazaji wa kipindi cha majadiliano cha kila siku (Jumatatu hadi Alhamisi) With Tigran Keosayan kilichorushwa na kituo cha televisheni binafsi cha REN-TV nchini Urusi.

Alifunga ndoa na Margarita Simonyan, mhariri mkuu wa kituo cha utangazaji kinachodhibitiwa na serikali ya Urusi, RT, pamoja na kundi la vyombo vya habari la serikali Rossiya Segodnya.

Keosayan alikuwa na matatizo ya moyo, akapata mashambulizi mwaka 2008 na 2010. Mnamo Januari 2025 aliingia kwenye koma na hakupata fahamu tena hadi kufariki tarehe 26 Septemba 2025.

  1. "Чем запомнился Тигран Кеосаян". Kommersant. 2025-09-26. Iliwekwa mnamo 2025-09-27.
  2. "«Сильный духом человек и настоящий патриот России»: Путин выразил соболезнования в связи со смертью Тиграна Кеосаяна". business-gazeta.ru. 2025-09-26. Iliwekwa mnamo 2025-09-27.
  3. "Russian News, English Accent". cbsnews.com (kwa American English). 11 Desemba 2005. Iliwekwa mnamo 18 Machi 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Ioffe, Julia (Septemba–Oktoba 2010). "What is Russia Today?". Columbia Journalism Review.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Margarita Simonyan biography Archived 21 Juni 2012 at the Wayback Machine, NewsExchange.org, accessed 20 September 2012.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tigran Keosayan kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.