Nenda kwa yaliyomo

Thomas Partey

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Thomas Partey

Thomas Teye Partey (alizaliwa Juni, 1993) ni mchezaji wa soka wa Ghana, ambaye anacheza kama kiungo mkabaji katika klabu ya Uingereza, itwayo Arsenal FC na timu ya taifa ya Ghana.

Atletico Madrid[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa huko Odumase Krobo, Thomas alikuwa Mchezaji wa klabu ya Odometah FC ya vijana. Baadaye alisaini mkataba na klabu ya Atlético Madrid mwaka 2011.Tarehe 10 Machi 2013, Thomas aliitwa katika kikosi cha kwanza cha Atlético Madrid katika mechi dhidi ya Real Sociedad.

RCD Mallorca[hariri | hariri chanzo]

Mnamo tarehe 12 Julai, Thomas alisajiliwa katika klabu ya kwa RCD Mallorca kwa mkopo, Mnamo 18 Agosti alicheza mechi yake ya kwanza,ambayo walifungwa goli 4-0 dhidi ya CE Sabadell FC

UD Almería[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 27 Julai 2014 Thomas alijiunga na La Liga huko Hispania katika klabu ya UD Almería. Alicheza mechi ya kwanza katika mashindano 23 Agosti mechi dhidi ya RCD Espanyol na kutoka sare ya goli 1-1.

Atletico Madrid[hariri | hariri chanzo]

Alichezea timu yake ya kwanza kwa mara nyingine Atletico tarehe 28 Novemba 2015, katika mechi ambayo walipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Espanyol.

Mnamo 2 Januari mwaka uliofuata aliisaidia klabu yake katika mechi dhidi ya Levante UD. Mnamo tarehe 28 Mei, Thomas alicheza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA dhidi ya Real Madrid.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Thomas Partey kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.