Nenda kwa yaliyomo

Thomas Garnet

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Thomas Garnet, S.J. (Southwark, 1575 hivi – Tyburn, 23 Juni 1608) alikuwa padri Mjesuiti kutoka Uingereza aliyeuawa kwa kuwa Mkatoliki chini ya mfalme James I[1].

Baada ya kusoma huko Ufaransa na Hispania, alipadrishwa akarudi Uingereza (1599) alipofanya utume kwa kificho miaka 6 hadi alipokamatwa kwa mara ya pili. Miezi baadaye alifukuzwa nchini kwa tishio la kuuawa akirudi tena.

Alipomaliza unovisi katika shirika huko Louvain, alitumwa Uingereza alipokamatwa wiki 6 tu baadaye akauawa kwa kukataa kiapo cha kumtii mfalme badala ya Papa[2].

Alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenyeheri tarehe 15 Desemba 1929, na Papa Paulo VI kuwa mtakatifu mfiadini tarehe 25 Oktoba 1970.

Sikukuu yake ni tarehe 23 Juni [3]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Pollen, John Hungerford, "Ven. Thomas Garnet", Catholic Encyclopedia (1913), juz. la Volume 6, iliwekwa mnamo 2018-08-22 {{citation}}: |volume= has extra text (help)
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/59100
  3. Martyrologium Romanum
  • POLLEN, "Protomartyr of Stonyhurst College" in Stonyhurst Magazine (1889), 334-82
  • BLACKFAN, Annales Coll. S. Albani, Vallesoleti, ed. POLLEN (1899), 57, 84
  • CAMM in The Month (Aug., 1898), 164-77
  • YEPEZ, Persecucion de Inglaterra (Madrid, 1599), 820-30
  • FOLEY, Records S.J., II, 475-505.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.