Nenda kwa yaliyomo

Thomas Baty

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Thomas Baty (8 Februari 18699 Februari 1954) alikuwa mwanasheria wa kimataifa, mwandishi na mtetezi wa usawa wa kijinsia na haki za wanawake kutoka Uingereza. Alisomea sheria katika Chuo Kikuu cha Oxford na kile cha Cambridge, na baadaye akawa mshauri wa kisheria wa serikali ya Japani kuanzia mwaka 1916. Baty alichapisha maandiko mengi kuhusu sheria za kimataifa na kwa jina lake lingine Irene Clyde aliandika riwaya ya Beatrice the Sixteenth, akianzisha pia jarida la Urania kupinga mgawanyo wa kijinsia. Akiwa Japani, alitetea sera za upanuzi wa nchi hiyo katika vikao vya kimataifa. Ingawa alishutumiwa na Uingereza kwa usaliti, alinyang’anywa uraia badala ya kushtakiwa. Alifariki Ichinomiya, Chiba, akiheshimiwa na viongozi wa Japani.[1][2][3]

Maisha na kazi

[hariri | hariri chanzo]

Thomas Baty alizaliwa tarehe 8 Februari 1869 huko Stanwix, Cumberland, akiwa mtoto mkubwa wa William Thomas Baty na Mary (née Matthews). Baba yake, mtaalamu wa kutengeneza samani, alifariki Baty akiwa na umri wa miaka saba, jambo lililomfanya kuwa na ukaribu mkubwa na mama yake na dada yake.

Baty pia alifanya kazi zake za uandishi kwa jina la Irene Clyde, akijulikana kwa uanaharakati wa kupinga mfumo dume na mgawanyiko wa kijinsia. Alihoji uhalali wa biological sex, ndoa za kiasili na mfumo wa uzalishaji, huku akihimiza kuenzi mahusiano ya wanawake kwa wanawake.

Mwaka 1909, Clyde alichapisha riwaya ya Beatrice the Sixteenth, akiizungumzia nchi ya Armeria. Katika riwaya Beatrice the Sixteenth, Armeria ni nchi ya kufikirika ambako hakuna tofauti kati ya mwanaume na mwanamke. Watu wake wote wanaonekana kuwa na tabia za upole na huruma, ambazo mara nyingi huchukuliwa kama za kike. Wanaishi pamoja kwa mshikamano, wakishirikiana bila ubaguzi au mgawanyo wa jinsia.

Baty pia alikuwa mbaguzi wa nyama tangu umri wa miaka 19, akawa makamu rais wa Vegetarian Society ya Uingereza, na mwanachama wa Humanitarian League na Animal Defence and Anti-Vivisection Society.

  1. "Baty, Thomas". Who Was Who, 1951–1960: A Companion to Who's Who, Containing the Biographies of Those Who Died During the Decade 1951–1960 (kwa Kiingereza). Juz. la 5 (tol. la 2nd). London: A & C Black. 1964. uk. 78 kutoka Internet Archive.
  2. Weinbren, Dan (1994). "Against All Cruelty: The Humanitarian League, 1891–1919" (PDF). History Workshop (38): 86–105. ISSN 0309-2984. JSTOR 4289320. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka (PDF) kutoka chanzo mnamo 4 Novemba 2021. Iliwekwa mnamo 4 Novemba 2021.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Life Members". Animal Defence and Anti-Vivisection Society: Reports for 1933 and 1934 (PDF) (kwa Kiingereza). 1934. uk. 5.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Thomas Baty kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.