Thokozani Chimbe

Thokozani Chimbe ni mwanasheria na mtaalamu wa usalama wa mtandao wa Malawi, na ni mmoja wa wataalamu wakuu katika kuunda mfumo wa kisheria wa Malawi kuhusu usalama wa mtandao. Anahudumu kama Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria katika Mamlaka ya Mawasiliano ya Malawi (MACRA).
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Chimbe alipata Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Malawi. Baadaye alipata stashahada ya uzamili katika uandishi wa sheria kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Sheria nchini Uganda, na shahada ya uzamili katika sheria za kompyuta na mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Queen Mary, London.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Chimbe alianza kufanya kazi katika Mamlaka ya Mawasiliano ya Malawi (MACRA) mwaka 2004.
Mwaka 2023, Chimbe aliongoza kamati ya maandalizi ya Women and Girls in Cyber, (Wanawake na Wasichana katika Usalama wa Mtandao) mkutano unaohamasisha wanawake na wasichana kushiriki katika usalama wa teknolojia na kidijitali.
Mwaka 2024, alisaidia kuendesha mafunzo ya MACRA kuhusu Sheria mpya ya Ulinzi wa Taarifa ya Malawi. Katika siku ya wazi ya MACRA mwezi Agosti 2024, alitangaza kuwa muswada wa uhalifu wa mtandao ulikuwa umeandaliwa na ulikuwa karibu kuwasilishwa na kupitishwa katika kikao kijacho cha Bunge.
Chimbe ni mwanachama wa Jumuiya ya Wanasheria ya Malawi, Chama cha Wanasheria Wanawake cha Malawi,Mawakili wa Kimataifa kwa ajili ya Afrika (ILFA) na Mtandao wa Washauri wa Usalama wa Mtandao (CyAN).[1][2][3][4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.coe.int/en/web/cybercrime/-/thokozani-chimbe
- ↑ https://www.nyasatimes.com/womens-cyber-platform-impressed-with-participation-at-the-meet/
- ↑ https://africabrief.substack.com/p/macra-trains-media-on-new-data-protection
- ↑ https://www.nyasatimes.com/macra-ready-with-cyber-crimes-bill/
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Thokozani Chimbe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |