The Roots
| The Roots | |
|---|---|
The Roots wakitumbuiza mnamo mwaka 2016 | |
| Taarifa za awali | |
| Chimbuko | Philadelphia, Pennsylvania, Marekani |
| Aina ya muziki | Hip hop, alternative rap, conscious rap, progressive soul, progressive rap |
| Miaka ya kazi | 1987–hadi sasa |
| Studio | Def Jam, DGC, Interscope Geffen A&M, MCA, Okayplayer |
| Ameshirikiana na | Nouveau Riche, Soulquarians |
| Wavuti | theroots.com |
The Roots ni bendi ya muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani iliyoundwa mnamo mwaka 1987 na mwimbaji Tariq "Black Thought" Trotter pamoja na mpiga ngoma Ahmir "Questlove" Thompson huko Philadelphia. The Roots wanafanya kazi kama bendi ya mjengoni (house band) kwenye kipindi cha televisheni cha chaneli ya NBC kiitwacho The Tonight Show Starring Jimmy Fallon, baada ya kuhudumu katika nafasi hiyo hiyo kwenye kipindi cha Late Night with Jimmy Fallon kuanzia mwaka 2009 hadi 2014. Wanachama wa kudumu wa The Roots kwenye kipindi cha The Tonight Show ni Captain Kirk Douglas (gitaa), Mark Kelley (besi), James Poyser (vinanda), Ian Hendrickson-Smith (saksofoni), Damon "Tuba Gooding Jr." Bryson (subesimbi/sousaphone), Stro Elliot (vinanda na ngoma), Dave Guy (honi/lipenenga), Kamal Gray (vinanda), na Raymond Angry (vinanda).
The Roots wanajulikana kwa mtindo wao wa hip hop wenye mchanganyiko wa jazz na midundo ya kipekee inayohusisha upigaji wa vyombo vya muziki vya mubashara,[1] na kazi za kundi hili zimekuwa zikikosolewa na kusifiwa sana kwa ubora wake. Mtandao wa ThoughtCo uliweka bendi hii katika nafasi ya 7 kwenye orodha ya Makundi 25 Bora ya Hip-Hop ya Muda Wote, ukiwaita "Bendi ya kwanza halisi ya hip-hop."[2]
Pamoja na muziki wa bendi hiyo, wanachama kadhaa wa The Roots wanajihusisha na miradi ya pembeni, ikiwa ni pamoja na utayarishaji wa muziki, uigizaji, na kushiriki mara kwa mara kama wasanii waalikwa kwenye albamu za wasanii wengine na kwenye matamasha ya mubashara.
Historia ya bendi
[hariri | hariri chanzo]1987–1993: Miaka ya awali
[hariri | hariri chanzo]
The Roots walianzia huko Philadelphia kupitia Ahmir "Questlove" Thompson na Tariq "Black Thought" Trotter walipokuwa wakisoma pamoja katika shule ya sekondari ya Philadelphia High School for the Creative and Performing Arts.[3] Walikuwa wakitumbuiza barabarani kwenye pembe za mitaa huku Questlove akipiga ndoo kama ngoma na Black Thought akichana mistari juu ya midundo hiyo. Onyesho lao la kwanza rasmi lilikuwa la kusaka vipaji shuleni mnamo mwaka 1989 ambapo walitumia jina la Radio Activity, ambalo lilikuwa mwanzo wa mfululizo wa mabadiliko ya majina yaliyopitia Black to the Future na baadae The Square Roots.[4] Rapa mwingine, Malik B., na mpiga besi wa kudumu, Leonard "Hub" Hubbard, waliongezwa kwenye bendi kabla ya kutoka kwa albamu yao ya kwanza. Mnamo mwaka 1992, waliondoa neno "Square" na kubaki "The Roots" kwa sababu kundi lingine la muziki wa asili la eneo hilo lilikuwa na hakimiliki ya jina hilo.
Baada ya kushindwa kupata mafanikio makubwa katika mji wao wa nyumbani wa Philadelphia, bendi hiyo ilihamia London kwa muda mfupi, ambako walitoa albamu yao ya kwanza ya mwaka 1993, Organix. Albamu hii ilitolewa na kuuzwa kwa kujitegemea. Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, bendi hiyo ilitengeneza kundi kubwa la washabiki waaminifu barani Ulaya, jambo lililochochewa na ziara zao za matamasha. The Roots walianza kupata ofa kutoka kwa lebo mbalimbali za muziki, na hatimaye bendi hiyo ilisaini mkataba na DGC/Geffen.
1994–1997: Do You Want More?!!!??! na Illadelph Halflife
[hariri | hariri chanzo]Albamu ya kwanza ya The Roots chini ya lebo ya DGC, Do You Want More?!!!??!, ilitolewa nchini Marekani mwaka mmoja baada ya kusaini mkataba huo. Wakati wa mchakato wa kurekodi, mwanamuziki wa beatbox Rahzel na mpiga vinanda Scott Storch walijiunga na bendi.[5] Kuongezeka kwa wanachama hawa wawili kuliongeza vionjo na ukubwa wa sauti ya bendi hiyo, na kuongeza hamasa kwenye vipindi vyao vya kupiga muziki huko Philadelphia, ambavyo bendi hiyo ilikuja kuvitumia kama sampuli za nyimbo kwenye albamu ya Do You Want More?!!!??!. Wimbo wa utangulizi wa albamu hiyo unamwonyesha Black Thought akitambulisha mtindo wao wa muziki kama "organic hip hop jazz"; albamu hii inasifika kwa mchanganyiko wa mtindo wa kisasa wa hip hop wa East Coast hip hop na vionjo vya jazz, ikitegemea sana vinanda vya Fender Rhodes vya Storch na saksofoni ya mwanamuziki mualikwa Steve Coleman. Albamu ilitoa nyimbo tatu zilizosindikizwa na video zake: "Proceed", "Distortion to Static", na "Silent Treatment". Albamu ilipata mafanikio ya kiasi miongoni mwa mashabiki wa muziki mbadala (alternative hip hop), huku ikisaidiwa zaidi na kuonekana kwa kundi hilo kwenye tamasha la Lollapalooza. Mnamo mwaka 1995, bendi hiyo ilitumbuiza kwenye Tamasha la Jazz la Montreux (Montreux Jazz Festival). Katika miaka iliyofuata tangu kutoka kwake, Do You Want More?!!!??! imekuja kuchukuliwa kama albamu ya kihistoria na ya kisasa ya jazz rap.[6]

Albamu ya mwaka 1996 ya Illadelph Halflife ilikuwa albamu ya tatu ya kundi hilo na ikawa ya kwanza kuingia kwenye 40 bora ya chati za Billboard 200,[5] ikichangiwa kwa kiasi fulani na kituo cha MTV kucheza video ya wimbo wa "What They Do" (ambao ulikuwa ukiiga na kufanyia dhihaka mambo yaliyozoeleka kwenye video za rap)[7] na wimbo wa "Clones", ambao ulikuwa wimbo wao wa kwanza kufika tano bora kwenye chati za rap. Wimbo wa "What They Do" pia ulikuwa wimbo wa kwanza wa kundi hilo kuingia kwenye Top 40 ya chati za Billboard, ukishika nafasi ya 34. Scott Storch aliondoka kwenye bendi na nafasi yake kuchukuliwa na mpiga vinanda mpya, Kamal Gray. Mtindo wa sauti wa bendi hiyo ulichukua mwelekeo wa giza zaidi katika kipindi hiki, ukiwa umechochewa sana na kundi la the Wu-Tang Clan pamoja na mtindo wa utayarishaji wa RZA uliokuwa wa chini na wa kuvutia, ukiwa umejaa sampuli kutoka kwenye muziki wa zamani wa jazz na muziki wa klasiki. Albamu hii pia inajulikana kwa kushirikisha wasanii wengi na washirika wa karibu, akiwemo Common, D'Angelo, Q-Tip, na wengineo. Ushirikiano huu ulitoa msingi wa kuundwa kwa kundi la Soulquarians na kukuza uhusiano wa The Roots na mtindo mdogo wa muziki wa neo-soul.
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]Albamu za studio
[hariri | hariri chanzo]- Organix (1993)
- Do You Want More?!!!??! (1995)
- Illadelph Halflife (1996)
- Things Fall Apart (1999)
- Phrenology (2002)
- The Tipping Point (2004)
- Game Theory (2006)
- Rising Down (2008)
- How I Got Over (2010)
- Undun (2011)
- ...And Then You Shoot Your Cousin (2014)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Powell, Kevin (Oktoba 24, 1996). "Album Review: Illadelph Halflife". Rolling Stone. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Mei 6, 2007. Iliwekwa mnamo Januari 25, 2010.
{{cite magazine}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Adaso, Henry (Oktoba 12, 2017). "25 Greatest Hip-Hop Groups – Best Rap Groups of All Time". ThoughtCo. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Agosti 13, 2018. Iliwekwa mnamo Machi 26, 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "The roots of Questlove's success". CBS News. Septemba 14, 2014.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Thompson, Ahmir 'Questlove'; Greenman, Ben (2013). "Chapter 9". Mo' Meta Blues: The World According to Questlove. Hachette Book Group. uk. 88.
- 1 2 Bush, John (2008). "The Roots – Biography". Allmusic. Iliwekwa mnamo Machi 3, 2009.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "The 10 Best Jazz Rap Albums To Own On Vinyl". Vinylmeplease.com. Novemba 4, 2016.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Roots Take A Swing At Video Cliches". MTV News. Januari 7, 1997. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Oktoba 30, 2001. Iliwekwa mnamo Machi 3, 2009.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi ya The Roots
- The Roots katika Allmusic
- Roots The Roots katika Discogs
- TheRootsArchive.com
- Uchambuzi wa The Roots katika DefJam
- Philadelphia ya kina The Roots katika MapQuest
