Nenda kwa yaliyomo

The Mechanic (filamu ya 2011)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka The Mechanic (2011 film))
The Mechanic

Picha ya tangazo la filamu
Imeongozwa na Simon West
Imetayarishwa na Irwin Winkler, Robert Chartoff, David Winkler, William Chartoff
Imetungwa na Lewis John Carlino (hadithi ya awali), Richard Wenk, Lewis John Carlino (toleo jipya)
Imehadithiwa na Richard Wenk
Nyota Jason Statham, Ben Foster, Donald Sutherland
Muziki na Mark Isham
Sinematografi Eric Schmidt
Imehaririwa na Todd E. Miller, Robert A. Ferretti
Imesambazwa na CBS Films
Imetolewa tar. 28 Januari 2011
Ina muda wa dk. Dakika 93
Nchi Marekani
Lugha Kiingereza
Bajeti ya filamu Dola milioni 40
Mapato yote ya filamu Dola milioni 76.3
Ikafuatiwa na Mechanic: Resurrection

The Mechanic ni filamu ya Marekani ya mwaka 2011. Ni filamu ya mapigano iliyoongozwa na Simon West. Waigizaji wakuu ni Jason Statham, Ben Foster, Tony Goldwyn, na Donald Sutherland.

Filamu hii ni toleo jipya la filamu ya mwaka 1972 yenye jina hilo hilo. Hadithi yake inamhusu Arthur Bishop (Statham), ambaye ni muaaji wa kulipwa. Kazi yake ni kuhakikisha kwamba mauaji anayofanya yanaonekana kama ajali au tukio la kujiua.

Filamu hii ilitolewa Marekani na Canada tarehe 28 Januari 2011. Watu walipenda sehemu za mapigano na jinsi Jason Statham alivyoigiza.

Mwaka 2016, sehemu ya pili ilitolewa kwa jina Mechanic: Resurrection, tarehe 26 Agosti.

Muaaji wa kulipwa, Arthur Bishop, anaingia kwa siri nyumbani kwa kiongozi wa genge la madawa ya kulevya la Colombia na kumzamisha katika bwawa lake mwenyewe. Akirudi nyumbani Louisiana, anakutana na rafiki yake na mwalimu wake, Harry McKenna.

Bishop anapewa kazi na mwajiri wake, Dean, ya kumuua Harry. Dean anamweleza Bishop kuhusu misheni iliyoshindikana nchini Afrika Kusini, ambapo mauaji kadhaa yalifanyika, huku taarifa za tukio hilo zikijulikana kwa Dean na Harry pekee. Kwa kusitasita, Bishop anamuua Harry na kufanya ionekane kama shambulio la unyang'anyi wa gari. Katika mazishi ya Harry, Bishop anakutana na Steve, mtoto wa Harry, ambaye baadaye anazuia kumuua mtu aliyekuwa akijaribu kuiba gari kwa hasira.

Steve anamwomba Bishop amfundishe kuwa muaaji wa kulipwa. Anapewa maagizo ya kumpeleka mbwa mdogo (Chihuahua) katika mgahawa wa kahawa kila siku, kwa muda maalum, ili kuvutia macho ya mlengwa wake, muuaji Burke. Kadri Steve anavyozoea ratiba hiyo, Bishop anampeleka kuangalia jinsi mauaji ya kulipwa hufanyika. Hatimaye, Burke anamwalika Steve kupata vinywaji.

Akipuuza maagizo ya Bishop ya kumpa Burke dawa ya kupoteza fahamu (Rohypnol), Steve anaenda naye nyumbani kwake. Burke anapoanza kuvua nguo, Steve anajaribu kumbana kwa mkanda, akimwiga Bishop. Burke anapambana naye, na Steve anafaulu kumua baada ya mapigano marefu. Dean anaonyesha kutopendezwa na jinsi Bishop alivyomshirikisha Steve, kinyume cha mkataba.

Shabaha inayofuata ya Bishop ni kiongozi wa kundi la ibada, Andrew Vaughn, ambapo Steve anapendekeza wampige sindano ya adrenalini ili kuonekana kama amepata mshtuko wa moyo, na madaktari wampatie dozi hatari ya epinephrine. Wakati Bishop na Steve wakijiandaa kumua, daktari wa Vaughn anafika na kumpa sindano ya ketamini, ambayo ingezuia athari za adrenalini. Hivyo, wanakubaliana kumziba pumzi badala yake.

Baada ya kumuua Vaughn, wanagunduliwa na walinzi, hivyo wanapigana kufa kupona kabla ya kutoroka kwa ndege tofauti. Bishop anapofika uwanja wa ndege, anagundua muuaji ambaye alipaswa kufa katika misheni ambayo Harry alihusishwa kimakosa. Muuaji anamweleza kuwa Dean alipanga njama hiyo kuficha mambo yake machafu. Bishop anagundua kuwa Dean alimfitini Harry na kwamba alimdanganya ili amuue Harry.

Baada ya kuangamiza watu wa Dean waliompiga mbinu, Bishop anatambua kuwa Steve amevamiwa katika nyumba ya maficho. Steve anaua washambulizi wake, anapata bastola ya baba yake, na anagundua kwamba Bishop alimuua Harry. Bishop na Steve wanamuua Dean kwa mvua ya risasi iliyochakaza wajihi wake. Wanaposimama kujaza mafuta, Steve analipua gari, akidhani Bishop yuko ndani.

Steve anarudi nyumbani kwa Bishop na anafanya mambo mawili ambayo Bishop alimkataza: Anacheza rekodi kwenye kifaa cha muziki na anachukua gari la Bishop—Jaguar E-Type ya 1966. Anapoondoka, Steve anaona karatasi kwenye kiti cha abiria ikisema: "Steve, ikiwa unasoma hii, basi umekufa."

Akigundua gari limesheheni bomu, Steve anacheka kwa mara ya mwisho kabla ya gari kulipuka na kumuua. Mlipo mwingine unaharibu nyumba ya maficho, kwani Bishop aliliandaa kujilipua ikiwa Steve angalicheza rekodi. Katika mazungumzo ya awali, Bishop aliona Steve akiweka bastola ya baba yake, jambo lililomhakikishia kuwa Steve aligundua ukweli.

Picha za kamera za usalama kwenye kituo cha mafuta zinaonyesha kuwa Bishop alitoroka kabla ya mlipuko. Anachukua gari jingine la akiba na kuondoka.

Waigizaji

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]