The Corruptor

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The Corruptor
Imeongozwa na James Foley
Imetayarishwa na Dan Halsted
Imetungwa na Robert Pucci
Nyota
Muziki na Carter Burwell
Junior Cyrus Baron
Imehaririwa na Howard E. Smith
Imesambazwa na New Line Cinema
Imetolewa tar. Machi 12, 1999 (1999-03-12)
Ina muda wa dk. 110 minutes
Lugha English
Cantonese
Bajeti ya filamu $25 million
Mapato yote ya filamu $24.5 million [1]

The Corruptor ni filamu ya mapigano iliyotoka 1999 nchini Marekani. Imeongozwa na James Foley. Waliocheza uhusika mkuu ni pamoja na Chow Yun-fat na Mark Wahlberg. Filamu ilitolewa nchini Marekani tarehe 12 Machi 1999,[2]

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Luteni wa NYPD, Nick Chen ni mkuu wa Kitengo cha Genge la Waasia, yaani, Asian Gang Unit (AGU). Kazi yake kubwa ni kutuliza ghasia zinazozuka katika mji wa Chinatown kati ya kundi la Tung Fung Benevolent Association na akina Fukienese Dragons, majambazi ya mtaani. Jambo linakuwa gumu kwa kile kilichokuwa kinaonekana kwamba Chen mwenyewe ni shushushu wa akina Tong chini ya uangalizi wa Uncle Benny Wong na luteni wake Henry Lee. Baada ya shambulio la bomu katika mji wa Chinatown, Chen anaungana na Danny Wallace bila kutaka, ambaye hakujua rushwa anazopiga Chen. Danny pia alikuwa akifanya kazi na Usalama wa Taifa kwa minajili ya kumchunguza Chen. Danny aliongopa kwa Chen na kundi zima la Kitengo cha Genge la Waasia kwa madai ya kwamba ameikubali kazi hiyo kwa lengo la kujipatia uzoefu wa kipelelezi haraka.

Wakati wa uvamizi wa polisi katika danguro la Fukienese, Chen anaokoa maisha ya Wallace. Wallace, kwa kufahamu ya kwamba sasa maisha yake yapo mikononi mwa Chen, anaanzisha uvamizi dhidi ya dawa za kulevya, tena kwa kufahamu kabisa kuna askari kanzu wa FBI anahusika katika uvamizi huo. Baada ya kuchimbwa mkwara wa kuingilia na upelelezi wao unaondelea, Wallace anatambulishwa kwa Lee. Lee anajadili umuhimu wa kuwa na askari mwengine ndani ya kundi la AGU juu ya wale wanaolipwa na Tong, jambo ambalo limeridhiwa na Uncle Benny. Benny anafanikiwa kumwingiza Wallace katika kumfanyia kazi kwa kumpa habari juu ya genge la uchangudoa lisilojulikana. Wallace anapewa dili kubwa la kumpa sifa, lakini Chen anaingiwa na wasiwasi huenda Wallace anafanya kazi na akina Tongs.

Wallace na Chen wanaingiliana katika mambo yao, wanauweka rehani urafiki wao na kujiebebesha maswali mengi juu ya dhamira ya Lee. Chen hawapendi akina Fukienese, lakini si yeye wala Danny anajua kama Lee anajenga uhusiano wa karibu na kiongozi wao—Bobby Vu. Wote Lee na Vu wanajua kama kuna kachero wa FBI ndani ya kundi lao la kijambazi na kuamua kuutwaa uhai wake.

Wakati wakichungua kwa karibu operesheni ya dawa za kulevya, Wallace na Chen wanashuhushudia vurumai iliyoletwa na kikosi cha Tong—iliyopelekea Chen achunguzwe kwa kuingilia upelelezi wa FBI. baada ya tukio, wote Wallace na Chen wanakubaliana kutoongea na FBI moja kwa moja bila kuwasiliana kwanza. Katika hangai zao, FBI wanagundua sababu kuu iliyopelekea Wallace kujiunga na AGU na kutishia kulipua siri yake au akubali amchunguze Chen kwa jicho la tatu. Wakati moja kati ya mashushu wa Chen akishuhudia Vu akimwua Uncle Benny, Chen anawapa taarifa akina DA, ambao wananuia kudhibiti akina Tongs chini ya RICO. Akina DA, FBI, Wallace na Chen wote wanaamua kutaka kumkamata Vu na kundi lake.

Katika hali isiyo ya kawaida, Lee anaamua kumjulisha Chen juu ya kazi yake halisi ya Wallace. Wakati wa opereshani ya usiku, Chen anatoa bastola yake na kumnyooshea Wallace akiwa na hasira nzito. Wallace anamalizana na Chen na hatimaye wakapambana na akinaDragons, wakawauwa wengi sana. Katika mapambano mengine mbele, Chen anamsukuma Wallace nje ya njia na kujikuta akipigwa risasi kali na Vu. Kisha Wallace anampiga risasi Vu na kufa papo hapo. Wakati hospitali, Wallace anakataa kuondoa kalima yake juu ya Chen kafa kama askari mzuri. Baadaye, Wallace anaongoza msafara wa askari kwenda kumkamata Lee. Chen anapewa maziko ya kishujaa huku Wallace akiongoza msafara.

Washiriki[hariri | hariri chanzo]

Mapato[hariri | hariri chanzo]

The Corruptor ilipata jumla ya kiasi cha dola za Kimarekani $24,493,693 kwa hesabu ya dunia nzima, ikiwa pamoja na $15,164,492 pekee kutoka Marekani na $9,329,109 kutoka katika nchi nyingine.[1]

Kibwagizo[hariri | hariri chanzo]

Kibwagizo cha filamu ya The Corruptor kina nyimbo za underground hip hop kutoka kwa wasanii kama vile Mobb Deep, Spice 1 na Mystikal. Muziki wa filamu ulitungwa na Carter Burwell.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 "The Corruptor". Box Office Mojo. Iliwekwa mnamo 2020-04-20. 
  2. "Corruptor, The (1999) - Overview". TCM.com. Iliwekwa mnamo 2012-07-18. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu The Corruptor kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.