The Best

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
“The Best”
“The Best” cover
Single ya Tina Turner
A-side 1. The Best
B-side 2. Undercover Agent For The Blues
3. Bold And Reckless
Imetolewa 2 Septemba 1989
Urefu 4:09
Studio Capitol Records
Mtunzi Mike Chapman, Holly Knight
“(Simply) The Best”
“(Simply) The Best” cover
Single ya Tina Turner & Jimmy Barnes
Imetolewa 1992
Urefu 4:11
Studio Mushroom Records
Mtunzi Mike Chapman, Holly Knight
Mwenendo wa Single za Tina Turner singles
Hide Your Heart

"The Best" ni wimbo uliotungwa na Mike Chapman na Holly Knight, ambao awali ulishirikishwa katika albamu ya Bonnie Tyler ya 1988 Hide Your Heart.

Wimbo huu, hatimaye, ulitayarishwa na kutolewa kama Single ya ufanisi mkubwa na Tina Tunner mnamo 1989 katika hit albamu yake Foreign Affair. Suti ya Saksafoni ya solo katika toleo la Turner inachezwa na Edgar Winter.

"The Best" ni miongoni mwa single za Turner zenye ufanisi mkubwa duniani, ikifikia kilele katika nafasi ya 15 katika chati za US Billboard 100 na ikafanikiwa kuingia katika tano bora za Ufalme wa Muungano, ikifikia kilele katika nafasi ya 5 na nchini Ujerumani ikafika #4. Matoleo Fulani ya Single ya Tina Turner pia yalishirikisha kibao kisicho katika albamu cha "Bold and Reckless", kilichotayarishwa na Rupert Hine.

Toleo lililorekodiwa na kwa ushirikiano na Jimmy Barnes, lililopewa jina "Simply the Best", lilikuwa hit single katika chati za Top 40 nchini Australia ambapo ilitumiwa katika kampeni za Ligi ya Rugby ya New South Wales.

Katika Utamaduni wa Pop[hariri | hariri chanzo]

"The Best" ilikuwa hata maarufu zaidi nchini UK kuliko US, ikiwa muziki wa kiingilio wa aliyekuwa Bingwawa dunia wa masumbwi kutoka Britain Chris Eubank. Pia ilikuwa wimbo wa kitambulisho wa aliyekuwa mwendeshaji magari wa Formula One wa Brazil Ayrton Senna. Toleo la Turner la wimbo huu linaonekana katika kipindi cha SingStar 80's cha PS2, na pia ulitumiwa katika sherehe za kustaafu kwa Pittsburgh Penguins, kwa Mario Lemieux, na pia ni sadfa kuwa jina la pili la Lemieux linamaanisha ‘’bora zaidi’’ (The best) katika Kifaransa

Wimbo huu ulichezwa katika PA system iliyofanyika Madison Square Garden wakati Mark Messier alikabidhiwa Kombe la Stanley baada ya ushindi wa New York Rangers dhidi ya Vancouver Canucks katika mechi ya saba ya Finali za Kombe la Stanley la 2004. Rangers waliusikiliza wimbo huo kabla ya mechi.[1]. Uliendelea kucheza huku Rangers wakiteleza kuzunguka barafu katika bustani na kombe hilo la Stanley.[2]

Toleo la Tyler la wimbo huo lilitumiwa katika video ya kumbukumbu kwa mwanamiereka wa WWE Edge ambayo ilipeperushwa mnamo 20 Julai 2007 katika kipindi cha ya WWE Friday Night SmackDown.

Seneta Joe Biden alitumia toleo la Turner katika kampeni zake za urais mnamo 2008.

Celine Dion amewahi kuuimba wimbo huo live katika tamasha za muziki.

Mwana miereka wa Japan, Osamu Nishimura leo hii huutumia wimbo huo kama muziki wake wa kiingilio.

Wimbo huu pia ni wimbo usio rasmi wa klabu ya Soka ya Rangers FC ya Scotland, ingawa wakati mwingine maneno ya ziada yanaweza kusikika.

Wimbo huu ulichezwa baada ya ushindi wote wa Buffalo Bisons wa nyumbani ukianzia pambio.

Matoleo na remix (Toleo la Tina Turner)[hariri | hariri chanzo]

  • 7" Edit - 4:11
  • Album Version Pia huitwa Extended 12" Mix - 5:28
  • Extended Mighty Mix - 6:35
  • Single Muscle Mix - 4:16
  • Extended Muscle Mix - 5:28
  • "(Simply) The Best" (pamoja na Jimmy Barnes, 1992) - 4:11
  • "(Simply) The Best" (Extended Mix) (pamoja na Jimmy Barnes, 1992) - 5:29

Unawili katika Chati[hariri | hariri chanzo]

Bonnie Tyler

Kilele Chati (1988)
10 Norway [1]
95 UK [2]
34 Spain [3]

Toleo la Tina Turner

Kilele Chati (1989)
2 Austrian Singles Chart
2 Polish Singles Chart
2 Spanish Singles Chart
3 Swiss Singles Chart
4 Australian Singles Chart
4 Canadian Singles Chart
4 German Singles Chart
4 Irish Singles Chart
5 Dutch Singles Chart
5 Norwegian Singles Chart
5 UK Singles Chart
6 US Rock Chart
7 Italian Singles Chart
11 Swedish Singles Chart
15 US Billboard Hot 100 Singles Chart
23 French Singles Chart

Toleo la Tina Turner & Jimmy Barnes

Kilele Chati (1992)
13 Australian Singles Chart

Virejeleo[hariri | hariri chanzo]

  1. New York Rangers Hockey: Game 7 of the 1994 Stanley Cup Finals. [television]. MSG Network. 1994-06-14. "Tina Turner's song, "Simply the Best," blaring over the loudspeakers. That's the song the Rangers listented to before the game."
  2. Hockey Night in Canada: Game 7 of the 1994 Stanley Cup Finals. [television]. CBC. 1994-06-14.