Teresia Wairimu
Mandhari
Teresia Wairimu Kinyanjuri (amezaliwa 15 Novemba 1957) ni mhubiri wa Injili kutoka Kenya, mwanzilishi na Mkurugenzi wa Faith Evangelistic Ministries (FEM). Ana zaidi ya washikirila 20,000 wa huduma hiyo, ikiwa na ofisi nchini Kenya, Marekani na Uingereza (UK). Alianzisha FEM mwaka 1989 wakati Makanisa ya Kipentekoste yalipoibuka kama mbadala wa ibada katika Madhehebu Makuu ya Kikristo. Wairimu alikuwa Muhubiri wa kwanza mwanamke kuendesha mikutano ya Injili ya Uamsho iliyofanyika katika viwanja vya Uhuru Park. Anatajwa kama mmoja wa waanzilishi wa kwanza wa mafundisho ya kupanda mbegu (Doctrine of Seed Planting-DSP) katika historia ya uinjilisti wa Kenya.[1][2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |