Tembo (samaki)
Mandhari
| Tembo | ||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Tembo milia-hanamu (Pristipomoides zonatus) | ||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
| Ngazi za chini | ||||||||||||
|
Jenasi 6; spishi 27, 10 katika Afrika ya Mashariki:
|
Tembo ni samaki wa baharini wa jenasi mbalimbali katika familia Lutjanidae ya oda Acanthuriformes katika ngeli Actinopterygii walio maarufu kwa matumizi. Wanatokea kwa kawaida katika maji ya kitropiki na kinusutropiki ya Bahari za Hindi na Pasifiki kwenye miamba ya matumbawe mpaka vina vya m 500. Hula samaki wengine, gegereka, ngisi na wanyama-koti.
Jenasi hizi ina spishi 27 duniani kote. Spishi 10 zimeriportiwa kutoka Afrika ya Mashariki.
Spishi za Afrika ya Mashariki
[hariri | hariri chanzo]- Aphareus furca, Tembo meno-madogo (Small-toothed jobfis)
- Aphareus rutilans, Tembo kutu (Rusty jobfish)
- Aprion virescens, Tembo kijani (Green jobfish)
- Macolor niger, Tembo kitubaku (Black-and-white snapper)
- Paracaesio xanthura, Tembo mkia-njano (Yellowtail blue snapper)
- Pinjalo pinjalo, Tembo pinjalo (Pinjalo snapper)
- Pristipomoides filamentosus, Tembo mwekundu (Crimson jobfish)
- Pristipomoides sieboldii, Tembo urujuani (Lavender jobfish)
- Pristipomoides typus, Tembo meno-makali (Sharptooth jobfish)
- Pristipomoides zonatus, Tembo milia-hanamu (Oblique-banded jobfish)
Picha
[hariri | hariri chanzo]- Tembo meno-madogo
- Tembo kutu
- Tembo kijani
- Tembo kitubaku
- Tembo mkia-njano
- Tembo pinjalo
- Tembo mwekundu