Nenda kwa yaliyomo

Telesphore Mkude

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Telesphore Richard Mkude)

Telesphore Mkude (amezaliwa Pinde, wilaya ya Mvomero, mkoa wa Morogoro, 30 Novemba 1945) ni askofu mstaafu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania.

Alipata upadrisho tarehe 16 Julai 1972.

Aliwekwa wakfu na Kardinali Laurean Rugambwa tarehe 26 Aprili 1988 kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Tanga.

Tangu tarehe 5 Aprili 1993 hadi tarehe 30 Desemba 2020 alikuwa askofu wa Jimbo la Morogoro. Ndipo alipostaafu kwa sababu ya umri.

Awali alihudumu kama Askofu wa Jimbo la Tanga kuanzia tarehe 18 Januari 1988 hadi 5 Aprili 1993. Alipewa uteuzi kuwa askofu na Papa Yohane Paulo II tarehe 18 Januari 1988.[1]

  1. David M. Cheney (4 Agosti 2024). "MicroData Summary for Bishop Telesphore Richard Mkude (born 30 November 1945), Bishop Emeritus of Morogoro". Catholic-Hierarchy.org. Kansas City. Iliwekwa mnamo 13 Januari 2025.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.