Tekirdağ

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 00:12, 10 Machi 2013 na Addbot (majadiliano | michango) (Bot: Migrating 42 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q182009 (translate me))

Tekirdağ ni mji uliopo Thrace ya Mashariki, katika sehemu ya Kiulaya, Uturuki. Huu ni mji mkuu wa Jimbo la Tekirdağ na unaonekana na wengi kama mji ni mdogo sana, mji mtulivu sana kuliko kituo chake cha kibaishara cha Çorlu, ambapo ndipo kuna makao makuu ya serikali. Idadi ya wakazi kwa mujibu wa sensa ya mwaka wa 2008 ilikuwa 137,962[1].

Mji wa Tekirdag ulipewa majina tofauti kabla haujapata jina lake la sasa. Ulikuwa ukijulikana kama “Rodosto” wakati wa zama za Byzanti, “Rodoscuk” baada ya kuangukia katika ufalme wa Osmani kunako karne ya 14. Baadaye ilipata jina karibu linalofanana na hili la sasa kunako karne ya 18: “Tekfurdag”... Ulianza kuitwa “Tekirdag” baada ya kutangazwa kwa Jamhuri.

Marejeo

Viungo vya Nje


Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tekirdağ kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.