Tejumade Alakija
Omoba Tejumade Alakija (17 Mei 1925 - Agosti, 2013) alishika nafasi ya mtumishi wa umma wa Nigeria ambaye alipanda cheo hadi cheo na kufikia kuwa mkuu wa kwanza mwanamke wa utumishi wa umma wa Jimbo la Oyo, Nigeria.
Alihudhuria shule ya msingi huko Ile Ife, shule ya sekondari ya chini katika Shule ya Wasichana ya Kudeti, Ibadan, kisha akaendelea hadi Shule ya Wasichana ya CMS Lagos kukamilisha elimu yake ya sekondari.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Binti malkia Alakija alizaliwa tarehe 17 Mei 1925 kwa baba yake, Adesoji Aderemi, Ooni wa Ife, huko Ile-Ife, Jimbo la Oyo kusini-magharibi mwa Nigeria . Alipata mansomo ya Shule ya Msingi na ya Sekondari ya Aiyetoro huko Ile-Ife, bnaada ya hapo Shule ya Wasichana ya Kudeti huko Molete, Ibadan kwa lengo ya elimu yake ya sekondari. Akiwa kwenye safari ya masomo yake, Alakija alikamilisha shahada yake ya kwanza juu ya historia kwenye Chuo cha Westfield ikiwemo ndani ya Chuo Kikuu cha London, Uingereza. [1] Alipata elimu ya kuwa mwalimu, na alikamilisha shahada yake ya Uzamili kwenye Chuo Kikuu cha Oxford kati ya mnamo 1950 na mnamo 1951, baada ya hapo akajiingiza kwenye utumishi wa umma wa Nigeria ambapo alielekezwa kufundisha. [2]
Alianza kazi yake ya ualimu kwenye Shule ya Malkia, Ede, Jimbo la Osun, na kisha akahamia Shule mpya ya Sekondari ya Wasichana ya Serikali mahali alipofanya kazi kuanzia mwaka wa 1951 hadi mwaka wa 1953. Enzi ya ufanyakazi wake kama mwalimu, aliunda shule yenye jina la Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Shule ya Sekondari mnamo wa 1953. Pamoja na haya alifanya kazi kwenye Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Biashara na Viwanda kama Katibu Msaidizi na alichaguliwa kwa nafasi ya Afisa wa Mafunzo anayeongoza Programu ya Mafunzo ya Utumishi wa Umma ya eneo hilo na katibu wa tume la msingi. Mtawalia kuanzia 1960 hadi 1964, na kisha, akawa Mkuu Afisa Uwekezaji kwenye Wizara ya Biashara na Viwanda anayehusika na Matangazo ya Viwanda kuanzia mnamo 1969 hadi mnamo 1972.
Binti mfalme Alakija pia alishika nafasi kwenye baadhi ya wizara za msingi, kama vile Wizara ya Afya kw nafasi ya Naibu Katibu Mkuu mnamo wa 1978, na pia kwenye Wizara ya Elimu kwa nafasi ya Katibu Mkuu mwaka wa 1979, kabla ya kuwa mkuu wa utumishi wa umma wa jimbo katika Jimbo la Oyo.
Alipanda cheo hadi chep na kupata afasi ya kuwa mkuu wa kwanza mwanamke wa utumishi wa umma wa Jimbo la Oyo . Kuanzia mwaka 1993 hadi mwaka 1997, alikuwa Pro-Chansela wa Chuo Kikuu cha Abuja . [3]
Binti mfalme Alakija alifariki katika Hospitali ya Chuo Kikuu, Ibadan mwaka wa 2013.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Oyo's First Female Head of Service, Princess Tejumade Alakija Dies at 88!". The Street Journal (kwa American English). 2013-08-23. Iliwekwa mnamo 2025-04-01.
- ↑ Professor Henry Louis Gates Jr.; Professor Emmanuel Akyeampong; Mr. Steven J. Niven (2 Februari 2012). Dictionary of African Biography. OUP USA. uk. 155. ISBN 978-0-19-538207-5.
{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Professor Henry Louis Gates Jr.; Professor Emmanuel Akyeampong; Mr. Steven J. Niven (2 Februari 2012). Dictionary of African Biography. OUP USA. uk. 155. ISBN 978-0-19-538207-5.
{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)Professor Henry Louis Gates Jr.; Professor Emmanuel Akyeampong; Mr. Steven J. Niven (2 February 2012). Dictionary of African Biography. OUP USA. p. 155. ISBN 978-0-19-538207-5.