Tegla Loroupe
Tegla Loroupe ni mwanariadha na mwanaharakati wa usalama, elimu, na haki za wanawake wa Kenya.
Loroupe alikuwa mwanamke Mwafrika wa kwanza kushinda Marathoni ya jiji la New York katika mwaka 1994 na aliweka rekodi ya ulimwengu ya marathoni.[1] Tegla Loroupe aliweka rekodi ya ulimwengu ya marathoni kutoka 19 Aprili 1998 hadi 30 Septemba 2001. Yeye bado ana rekodi ya ulimwengu kwa mashindano ya kilometa 25 na 30. Yeye alishinda shindano katika miji ya London, Boston, Rotterdam, Hong Kong, Berlin, Rome na miji mwingine.[2] Katika 2003, Loroupe aliunda taasisi ya fedha ya kuchangia amani na usalama ambayo inaitwa Tegla Loroupe Peace Foundation Archived 24 Julai 2019 at the Wayback Machine.. Kisha katika 2006, yeye aliunda mbio za Amani na Usalama za kilometa 10. Aidha, Loroupe alianzisha timu ya wakimbizi katika Olimpiki ya 2016.[3]
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Tegla Loroupe alizaliwa katika kijiji cha Kutomwony, jimbo la Pokot Magharibi. Mama na Baba yake wanatoka kabila la Pokot. Yeye alikuwa na kaka na dada ishirini na nne. Baba yake alikuwa na wake wanne. Loroupe alifanya kazi katika shamba la familia na alitunza watoto. Baba yake alimwita yeye bozibozi kwa sababu baba yake alifikiri kwamba wanawake walikuwa bozibozi.[4] Ili aweze kwenda shule, Tegla alikimbia kilometa kumi kwenda shuleni na kurudi nyumbani. Yeye hakuvaa viatu. Shuleni, yeye aligundua kwamba yeye alikuwa mkimbiaji mzuri na alishinda mashindano. Loroupe alishinda mashindano ya nchi akiwa hajavaa viatu katika mwaka 1988. Baadaye, yeye alijielimisha kwa dhati.[5] Katika mwaka 1994, Loroupe alishinda Mashindano ya "Goodwill Games” na Marathoni ya jiji la New York. Yeye alishinda Marathoni ya jiji la New York tena katika mwaka 1995 na “Goodwill Games” katika mwaka 1998.[6] Tegla Loroupe aliendelea kushinda mashindano muhimu ya marathoni.[3]
Uanaharakati
[hariri | hariri chanzo]Tegla Loroupe amefanya kazi kubwa kuleta amani katika nchi ya Kenya na dunia nzima. Mkufo wa fedha wa Tegla Loroupe na Mbio za Amani vimeleta watu wanasiasa na watu wa makabila tofauti pamoja. Mbio za Amani katika mwaka 2006 zilikuwa na wakimbiaji elfu mbili kutoka makabila sita. Yeye alianzisha chuo cha masomo ya amani cha Tegla Loroupe kilichopo jijini Nairobi. Katika mwezi wa kumi na mbili, mwaka 2006, yeye alisafiri na watu maarufu hadi miji mikubwa kuzungumza kuhusu vita vya Darfur. Katika mwezi wa pili, mwaka 2007, Tegla Loroupe aliitwa Balozi wa Oxfam katika michezo na usalama wa Darfur.[7] Katika mwaka 2006, Loroupe aliitwa Balozi katika michezo na usalama wa Umoja wa Mataifa. Aidha, Loroupe alishinda Tuzo ya Wanawake ya michezo kutoka Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa katika mwaka 2011.[8] Loroupe amekuwa balozi kwa Kombe la Watu Bila Makazi la Dunia kwa vile 2015.[9]
Katika mwaka 2016, timu ya Tegla Loroupe ya wakimbizi ilishiriki michezo ya Olimpiki kwa mara ya kwanza. Timu ya wakimbizi ya Olimpiki ilikuwa na wachezaji kumi. Wachezaji hao walitoka Sudani Kusini, Ethiopia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Syria.[10] Wachezaji watano walijiandaa katika kambi ya wakimbizi iliyoko karibu na Nairobi na walisimamiwa na Tegla Loroupe. Loroupe alisema, “Watu wanawachukulia wakimbizi kama majambazi. Tunahitaji kuwachukulia kwa heshima.”[4]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "ESPN.com - MORESPORTS - Loroupe sets women's marathon record". www.espn.com. Iliwekwa mnamo 2019-07-24.
- ↑ "https://www.nyrr.org/about/hall-of-fame/tegla-loroupe". www.nyrr.org (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-07-24.
{{cite web}}
: External link in
(help)|title=
- ↑ 3.0 3.1 "Tegla Loroupe", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2019-03-23, iliwekwa mnamo 2019-07-24
- ↑ 4.0 4.1 Longman, Jeré (2016-08-04), "Tegla Loroupe Gives Refugee Olympians a Lesson in Hope", The New York Times (kwa American English), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2019-07-24
- ↑ "Tegla Loroupe", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2019-03-23, iliwekwa mnamo 2019-07-24
- ↑ "Tegla LOROUPE | Profile | iaaf.org". www.iaaf.org. Iliwekwa mnamo 2019-07-24.
- ↑ "Oxfam Ambassador Tegla Loroupe visits Darfur". Oxfam NZ (kwa Kiingereza). 2007-07-18. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-24. Iliwekwa mnamo 2019-07-24.
- ↑ "Tegla Loroupe wins IOC Women and Sport World Trophy". International Olympic Committee (kwa Kiingereza). 2017-02-06. Iliwekwa mnamo 2019-07-24.
- ↑ "Tegla Loroupe". Homeless World Cup (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2019-07-24.
- ↑ "Refugee Olympic Team". International Olympic Committee (kwa Kiingereza). 2019-06-20. Iliwekwa mnamo 2019-07-24.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tegla Loroupe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |