Tefik Mborja
Tefik Selim Mborja (6 Novemba 1891 – 1 Julai 1954) alikuwa mwanasiasa na mwanasheria wa Albania. Alihudumu kama katibu mkuu wa Chama cha Kifashisti cha Albania wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.[1]
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Tefik Mborja alizaliwa mnamo mwaka 1888, huko Mborje, Vilayet of Monastir, chini ya Dola la Osmani (ambayo leo ni Albania).[2]
Mborja alikuwa mbunge katika kipindi cha kati ya vita kuu mbili za dunia (interbellum). Akiwa mpinzani mkubwa wa Ahmet Zogu, alimuunga mkono Fan Noli. Mborja alihudumu kama mwakilishi wa Noli mjini Roma tangu mwaka 1924. Alipewa jukumu la kuanzisha uhusiano wa kitalama na Umoja wa Sovyeti, na kwa sababu hiyo aliwasiliana na mwakilishi wa Sovyeti mjini Roma, Konstantin Juranev.[3] Alipokuwa Italia, alikua rafiki wa karibu wa familia ya Count Galeazzo Ciano.[1] Alisomea sheria (jurisprudence) mjini Roma.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 Fischer, Bernd Jürgen. Albania at War: 1939-1945. London: Hurst, 1999. pp. 45-46
- 1 2 Aliko, Tomor (2007), GENOCIDE ON THE INTELLECTUAL ELITE OF THE ALBANIAN NATION UNDER THE COMMUNIST TERROR (PDF), Tirana: Shtypshkronja "MALUKA", uk. 43, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2013-12-30, iliwekwa mnamo 2013-12-28
- ↑ Robert Clegg Austin (2012), Founding a Balkan State: Albania's Experiment with Democracy, 1920–1925, University of Toronto Press, uk. 138, ISBN 9781442644359
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tefik Mborja kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |