Nenda kwa yaliyomo

Teen Titans Go!

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Teen Titans Go! ni katuni inayohusu mashujaa watano ambao ni Robin,Beast Boy,Cyborg,Raven na Star Fire .Mashujaa hawa katika mji wao wanaoishi kama walinzi wa mji na huhakikisha usalama wa watu wanaoishi nao

Nguvu zao:

Robin - kama kiongozi wao - ana stadi za uchunguzi wa kesi tofauti kutokana na vipande tofauti vya habari,ana stadi za upiganaji wa karate kwa ajili ya kujilinda na kuwalinda watu wanaomzunguka na pia ana elimu juu ya utengenezaji wa vifaa kadha wa kadha vya kiteknolojia.

Kabla ya kuundwa kwa The Teen Titans Robin alikuwa msaidizi wa Bat man.

Beast Boy - ni mwana chama wa Teen Titans ambaye ana nguvu na uwezo wa kujibadilisha kuwa aina yoyote ya mnyama muda wowote .Beast Boy akiwa mwana chama mtundu zaidi ya wote wa Teen Titans mara nyingi Beast Boy hutoa msaada wa nguvu kuendana na aina ya wanyama anaoweza kuwa.

Cyborg- ni mmoja wapo kati ya wanachama waadilifu wa Teen titans ambaye ametengenezwa akiwa na robo tatu ya mwili wa roboti na robo iliyo katika sura yake ni binadamu.Cyborg ana faida nyingi katika kundi la Teen Titans kwa sababu ya uwezo wake wa kujiunga na mtandao wa aina yoyote.na pia ana uwezo wa kutengeneza aina yoyote ya silaha.

Raven- ni shujaa aliye tokea kuonekana na teen titans akiwa na nguvu ya kuendesha vitu tofauti vinavyo mzunguka na hata binadamu kitabia.amepata jina la raven kwa sababu ya nguvu yake maalum itotokanayo na kunguru ambaye huwasilisha ukoo wao.

Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Teen Titans Go! kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.