Teddy Teclebrhan
Tedros TeddyTeclebrhan (alizaliwa tarehe 1 Septemba 1983) ni mchekeshaji na muigizaji wa Kijerumani, anayejulikana zaidi kwa ucheshi wake wa jukwaani uitwao Teddy Comedy.
| Teddy Teclebrhan | |
|---|---|
| Amezaliwa | 1 Septemba 1983 Asmara, Ethiopia |
| Jina lingine | Antoine Burtz, Percy, Ernst Riedler, Carlos, Lohan Cohan |
| Kazi yake | comedian,muigizaji |
| Teddy Teclebrhan |
|---|
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Teclebrhan alizaliwa mjini Asmara, Ethiopia mwaka 1983 na alikuwa mtoto wa mwisho kati ya wana wa tatu.[1] Alikulia Mössingen, Ujerumani. Baada ya kumaliza huduma ya kijamii (Zivildienst), alijiunga na chuo cha kimataifa cha sanaa ya uigizaji, CreArte kilichopo Stuttgart, ambako alihitimu mwaka 2008.
Teclebrhan alionekana kwa mara ya kwanza kwenye televisheni mwaka 2009, akicheza kama mmiliki wa kituo cha mafuta kutoka Swabia katika kipindi Laible und Frisch kilichorushwa na mtandao wa SWR, na kama muuzaji wa dawa za kulevya kutoka Rhineland katika kipindi Stolberg kilichorushwa na ZDF.
Mwaka huo huo, 2009, Teclebrhan alifanya onyesho lake la kwanza jukwaani katika tamthilia ya muziki Hairspray.[2] Kuanzia Desemba 2009 hadi Septemba 2010, alicheza nafasi ya Seaweed J. Stubbs.
Alianza kupata umaarufu mkubwa kupitia video ya YouTube aliyopakia mwaka 2011 iitwayo Umfrage zum Integrationstest (was nicht gesendet wurde) (Uchunguzi wa mtihani wa ujumuishaji (vipande vilivyokatwa)"), ambapo alionekana kwa mara ya kwanza katika nafasi aliyoibuni mwenyewe iitwayo "Antoine".[3] Kufikia Novemba 2021, [4]video hiyo ilikuwa imeangaliwa zaidi ya mara milioni 42.
Mnamo Mei 2012, video za kwanza za kipindi chake cha jukwaani Teddy's Show zilianza kurushwa kwenye ZDFneo. Kipindi hicho kilijumuisha ucheshi wa kusimama jukwaani (stand-up comedy), bendi ya muziki ya moja kwa moja, na mazungumzo na wageni. Mbali na Antoine, Teclebrhan pia alicheza wahusika wapya alioibuni mwenyewe – "Percy", "Lohan Cohan", "Ernst Riedler" na "Ringo Fleischer".[5][6]
Mnamo Aprili 2012, alisherehekea uzinduzi na kuanza kwa ziara yake ya jukwaani ya vichekesho Teddy Show – Was labersch du…?! nchini Ujerumani, Austria na Uswisi.
Mwaka 2013, alichapisha mfululizo wa wavuti uitwao Bootcamp kwenye chaneli yake ya YouTube TeddyComedy.[7]
Katika filamu Half Brothers ya mwaka 2014 iliyoongozwa na Christian Alvart, Teclebrhan alicheza nafasi kuu pamoja na Fahri Yardım na Sido.[8]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Teddy Teclebrhan kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-01-16. Iliwekwa mnamo 2025-09-27.
- ↑ Tedros Teclebrhan
- ↑ Alle Inhalte von ZDFneo
- ↑ Integration test survey (which was not sent)
- ↑ Aktuelle Nachrichten und Kommentare - SZ.de
- ↑ 360 Grad: Was labert der? – Quotenmeter.de
- ↑ Antoine Boot Camp Nr.1 - YouTube
- ↑ Sido spielt Hauptrolle in Spielfilm "Unter Brüdern" - rap.de