Tatum Keshwar
Tatum Keshwar (alizaliwa Durban, 14 Desemba 1983) ni mwanamitindo, mwanasaikolojia, na mshindi wa mashindano ya urembo kutoka nchini Afrika Kusini.
Alitunukiwa taji la Miss South Africa 2008. Aliiwakilisha Afrika Kusini katika Miss Universe 2009, ambako aliingia kumi bora, na pia katika Miss World 2009, ambako alipata nafasi ya mshindi wa pili wa pili (second runner-up).[1]
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Keshwar alisoma katika shule ya Mowat Park Girls High na alipata shahada ya saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha KwaZulu-Natal. Mwaka 2007, aliingia fainali katika msimu wa tatu wa shindano la uhalisia la uanamitindo Revlon Supermodel, kabla ya kushinda taji la Miss South Africa tarehe 15 Desemba 2008.
Keshwar aliwakilisha nchi yake katika shindano la Miss Universe 2009 lililofanyika Nassau, Bahamas, ambapo aliingia fainali na kushika nafasi ya saba kwa jumla.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Walubengo, Peris (2019-11-18). "Was Tatum Keshwar also engaged to Duduzane Zuma?". Briefly (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-06-15.
- ↑ "Tatum Keshwar | TVSA". www.tvsa.co.za. Iliwekwa mnamo 2024-06-15.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tatum Keshwar kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |