Tatu Chafu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Tatu Chafu
Tatu Chafu filamu.jpg
Posta ya "Tatu Chafu"
Imeongozwa na Novatus Mugurusi (Rrah C)
Imetayarishwa na Prisca Emmanuely
Paul MashauriMtayarishaji Mtendaji
Jacqueline MgumiaMtayarishaji Mtendaji
Imetungwa na Novatus Mugurusi
Nyota Akbar T Manka
Jackson Kabirigi
Noriega Francis
Paul Katambo
Nkwabi Elias
James James
Levison James
Webiro Wassira
Faraj Mhando
Paul Katambo
Muziki na Tiddy Hotter
Sinematografi Hamisi Koba
Karabani-Karabani
Imehaririwa na Zachary Fredrick
Imesambazwa na BongoHoodz
Imetolewa tar. 16 Disemba, 2017(kwenye makumbi ya sinema)
1 Mei, 2018(katika Youtube)
Ina muda wa dk. 136
Nchi Tanzania
Lugha Kiswahili

"Tatu Chafu" ni jina la filamu ya uhalifu na usela iliyotolewa 16 Disemba 2017 kutoka nchini Tanzania. Filamu imeongozwa na Novatus Mugurusi na kutayarishwa na Prisca Emmanuely na Paul Mashauri kwa ushirikiano na Production X, Next Level, Nitron Studios, Clouds Plus, Makini Studio na Cheusi Dawa TV. Kazi kubwa imefanywa na Mashauri Studios, Novitech na Production X. Ndani yake anakuja Akbar T. Manka, Jackson Kabirigi, Noriega Francis, Paul Katambo, Nkwabi Elias, Meya Shabani, Webiro "Wakazi" Wassira, Faraji Mhando, James James, Levison James, Lupyana Kihaka, Hussein Msangi, Salum Khalid, Henry Filbert na Laban Dabo Mbibo.

Filamu inahusu maisha ya kudanga ya vijana watatu marafiki waliokuwa marafiki tangu utotoni. Wamekuwa wakiishi katika mazingira ya pamoja katika hali mbalimbali. Vilevile kushiriki katika harakati za uhalifu na dhulma kadha wa kadha. Marafiki hawa ambao ni Cheddah, Bambino na Rochi ambaye anaonekana kama mpanga madili yote na mwenye kujielewa kuliko wote katika kundi hili. Sehemu kubwa ya filamu inazungumzia madawa ya kulevya na bangi. Mihadarati na maisha ya uhalifu yametawala katika filamu.

Filamu imetengenezwa katika maeneo ya Dar es Salaam pekee. Filamu imesambazwa na BongohoodZ ambayo inatumia teknolojia ya kisasa katika usambazaji wa filamu. Awali kulikuwa na malalamiko mengi juu ya uibiwaji wa kazi za wasanii. Filamu imezinguliwa katika muundo wa kimatamasha ambapo kunakuwa na mambo mengi yanatolewa wakati filamu inaonyeshwa.[1][2]

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Filamu inaanza na Chedah (Jackson Kabirigi) na Bambino (Akbar Manka) wakimuuzia mtu viatu kanyaboya huku Rochi (Noriega Francis) akielezea namna wizi unavyofanyika. Rochi anajitambulisha kama mpenda kuvuta bangi, hadi wakati mwingine anavuta hadi mzigo anaouza. Wakati Bambino mtu wa mademu, mapenzi kwa maneno uthibitisho hakuna. Chedah mtu wa madili mengi na maneno chungumzima huku akiamini mdomo wake ndio hela yake. Maisha ya kila siku ya kubangaiza. Siku moja kuna mtu anakuja, Frank (Laban Dabo Mbibo), anawapa mchongo wa kutafuta madawa ya kulevya kuna mtu anayataka. Mpango kapewa Rochi, ambaye ana mahusiano ya kuuziana bangi na Frank. Rochi anapeleka mchongo kwa washikaji wajue wapi wanaweza kupata mali. Chedah anasema kuna mzee Mangele (Nkwabi Elias) anajulikana mtaani kama mwuzaji mkubwa wa dawa za kulevya. Bila kusita wanajitosa kwa Mangele, awali anaonekana kukataa kujihusisha na mambo ya dawa za kulevya. Lakini dau lililotajwa linamfanya kukubaliana na hali.

Rochi anaambiwa achukue mzigo kwenye jokofu, ndani yake kuna maiti ikiwa kama kitisho iwapo watajaribu kumdhulumu. Kawaambia wenzake, lakini hawajamwamini. Hali hii imempa mshituko mkubwa sana Rochi. Mzigo unachukuliwa tayari kwa mauzo, Frank anazingua hatokei kwa muda uliopangwa. Wanaamua kupoteza muda magetoni ili kusubiria simu ya Frank. Upande wa majambazi, waonekana kulaumiana juu ya jaribio la ujambazi lililofeli. Mkuu wa kitengo, Machete (Paul Katambo), mpayuko mwanzo mwisho. Anamlaumu Mbita (Hussein Msangi) kuleta gari lisilo na mafuta. Kifeda (Musa Mohamed) analaumiwa kwa kuacha mizigo.

Punde anaingia Uswege (Faraji Mhando) mwenye hasira juu ya tukio lililotokea na kufeli. Anawatisha na kuwaasa wakiendelea na ujinga wao watadakwa na kupotea mazima. Baada ya maneno ya kashfa, Uswege ambaye anaonekana ndiye mratibu wa matukio kibao. Anawagusia kuhusu mchongo mpya wa kuiba kiboksi chenye pete katika duka moja la sonara kwa Mpemba. Uswege anawaambia wakifanikisha wasimtafute. Yeye anajua wapi pa kuwapata. Huko magetoni, vijana wanacheza gemu kwenye TV, ghafula Mbita anagonga lango kama ugomvi, Bambino anakurupuka kwenda kumwaga dawa za kulevya chooni. Bila kujua aliyegonga ni Mbita ambaye kaja kununua bangi kwa Rochi. Kwa kigugumizi Bambino anasema kamwaga mzigo wa mzee Mangele.

Vijana wanajadili namna ya kumkabili Mangele. Hapa kitendawili kikubwa kisichoweza kuteguka. Mangele hana ngoma za kukaanga, anacheka usoni, moyoni ana kiza. La Familia wanatoka magetoni na kuanza kusakanya pesa zilipo.

Muziki[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]