Nenda kwa yaliyomo

Tammy Abraham

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tammy Abraham mwaka 2016 akiwa chelsea
Tammy Abraham katika mechi ya norwich dhidi ya Chelsea 2019

Kevin Tamaraebi Abraham (anayejulikana kama Tammy Abraham, alizaliwa 2 Oktoba 1997) ni mchezaji wa soka wa Uingereza ambaye anacheza kama mshambuliaji wa klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza iitwayo Chelsea F.C. na timu ya taifa ya Uingereza.

Kazi ya klabu[hariri | hariri chanzo]

Abraham alicheza kwa mara ya kwanza kwa mkopo katika klabu hiyo mnamo 2016 na baadaye kwenda katika klabu ya Bristol City na aliisaidia timu yake kumaliza katika nafasi nzuri, baadaye alipata tuzo ya mchezaji wa kwanza mdogo.

Baadaye alienda katika klabu ya Swansea City kwa msimu mmoja akiwa katika ligi daraja la kwanza akiwa na Swansea City aliweza kupanda hadi Ligi Kuu. Kisha akajiunga na Aston Villa mnamo 2018 na kuwa mchezaji wa kwanza tangu 1977 kufunga mabao 25 ​​klabu hiyo.

Kazi ya kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Abraham aliwakilisha taifa la Uingereza katika mashindano ya chini ya miaka 18, na alionekana tena katika Mashindano hayo ya Ulaya ya chini ya miaka 21 ya UEFA huko Poland.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tammy Abraham kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.