Nenda kwa yaliyomo

Tambarare ya Siberia Magharibi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mto Vasyugan.
Sehemu ya Magharibi ya Siberia katika ramani ya satelaiti ya Asia ya Kaskazini.

Tambarare ya Siberia Magharibi (kwa Kiingereza: West Siberian Plain) ni tambarare kubwa ambayo inachukua sehemu ya magharibi ya Siberia, kati ya Milima ya Ural upande wa magharibi na Mto Yenisei upande wa mashariki, tena Milima ya Altay upande wa kusini mashariki. Eneo lote ni takriban km² 2,500,000.

Miji muhimu ni pamoja na Omsk, Novosibirsk, Tomsk na Chelyabinsk.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Tambarare ya Siberia Magharibi jinsi inavyoonekana ukipita kwa reli ya Kuvukia-Siberia karibu na Tatarskaya.

Tambarare hii inafunika takribani theluthi moja ya Siberia nzima [1] ikienea kwa km 2,400 kutoka Bahari ya Aktiki hadi kwenye miinuko ya Milima ya Altay, na km 1,900 kutoka Milima ya Ural hadi Mto wa Yenisei.

Kuna sehemu pana za vinamasi. Upande wa kusini iko misitu ya misonobari, inayoendelea kubadilika kuwa misitu ya taiga, na hatimaye tundra kadiri inavyofika kaskazini zaidi ambako jotoridi inashuka. Katika maeneo hayo ya kaskazini mimea mirefu kama miti haiwezi kustawi kwa sababu ya upungufu wa maji ambayo yameganda kuwa barafu.

Mito mikubwa ni:

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Western Siberian Plain". Columbia Encyclopedia. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-28. Iliwekwa mnamo 2006-10-24.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tambarare ya Siberia Magharibi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.