Nenda kwa yaliyomo

Taitoa Wihone

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Taitoa Wihone (jina la kuzaliwa; Luke Leon Taitoa Wijohn; alizaliwa Februari 2002) ni mwanaharakati wa mazingira na mgombea wa kisiasa kutoka nchi ya Nyuzilandi.

Maisha ya Kibinafsi

[hariri | hariri chanzo]

Wihone alizaliwa mwezi Februari mwaka 2002. Yeye ni mtu wa asili ya Kimaori. Hivyo basi watu wake ni Ngāpuhi, Ngāi Tūhoe, na Te Rarawa.[1] Alihudhuria darasa linalofundisha kwa lugha ya Kimaori katika shule ya Richmond Road na baadaye alihudhuria chuo cha Western Springs, ambapo alikuwa nahodha wa timu ya hoki.[2][3] Mama yake Elisa Lavelle Wijohn alikuwa mtetezi wa watu wanaougua saratani ya matiti hadi kifo chake mwaka wa 2022.[4][5][6]

Harakati na Siasa

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2017, Wihone alijitolea katika kampeni ya uchaguzi ya Julie Anne Genter. Mnamo mwaka 2019, alisaidia kuongoza mgomo wa shule kwa ajili hali ya hewa huko Auckland, na watu wapatao 80,000 walijitokeza.[3] Alipokea tuzo ya balozi wa dhamiri kwa niaba ya harakati hiyo.[7]

Wihone alichaguliwa na Chlöe Swarbrick kushiriki katika bunge la vijana la nchi ya Nyuzilandi mwaka 2019. Wakati wa mjadala mkuu, aliwasilisha hoja ya kulitaka bunge la vijana litangaze dharura ya hali ya hewa. Hoja hiyo ilipitishwa ndani ya dakika mbili. Wihone na Wabunge vijana wengine wapatao 78 walitia saini barua ya wazi kwa wabunge wazima wakiwasihi pia kutangaza dharura ya hali ya hewa.[8][9]

Wihone alichaguliwa mwezi Februari mwaka 2020 kugombea nafasi ya ubunge katika eneo la Mount Albert katika uchaguzi mkuu wa Nyuzilandai wa mwaka 2020. Kati ya wagombea vijana kadhaa, alikuwa mdogo zaidi, akitimiza miaka 18 chini ya miezi 8 tangu uchaguzi huo. Kama ilivyo kwa wagombea wengi wa Chama cha Kijani, alikuwa akipiga kampeni kwa ajili kura ya chama.[3] Aliwekwa nafasi ya 18 kwenye orodha ya chama. Katika uchaguzi huo alishika nafasi ya tatu kwa 5.56% ya kura, na nafasi yake kwenye orodha haikuwa ya juu vya kutosha kuingia bungeni.[10][11]

Wihone anaunga mkono suala la kupunguzwa kwa umri wa kupiga kura na kuboresha elimu ya uraia mashuleni.[12] Anaunga mkono kodi ya utajiri na uhalalishaji wa bangi.[2]

  1. "Party profile: Green Party — NZ Election 2020". Your complete guide to NZ Election 2020 — Policy (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-08-22. Iliwekwa mnamo 2025-10-24.
  2. 1 2 "Ponsonby News - New Zealand". ponsonbynews.co.nz (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-02-18. Iliwekwa mnamo 2025-10-24.
  3. 1 2 3 "Stuff". www.stuff.co.nz. Iliwekwa mnamo 2025-10-24.
  4. "Pharmac funding should be doubled - breast cancer advocate", Newshub (kwa Kiingereza), 2019-03-13, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-01-16, iliwekwa mnamo 2025-10-24
  5. "'I want to see my children turn 21': Living with breast cancer". NZ Herald (kwa New Zealand English). Iliwekwa mnamo 2025-10-24.
  6. "Elisa LAVELLE WIJOHN Obituary (2022) - The New Zealand Herald". Legacy.com. Iliwekwa mnamo 2025-10-24.
  7. "Stuff". www.stuff.co.nz. Iliwekwa mnamo 2025-10-24.
  8. "Youth Parliament 2019 declares climate emergency". RNZ (kwa New Zealand English). 2019-07-18. Iliwekwa mnamo 2025-10-24.
  9. "Youth MPs send climate change hurry-up to MPs". RNZ (kwa New Zealand English). 2019-07-23. Iliwekwa mnamo 2025-10-24.
  10. "E9 Statistics - Electorate Status". www.electionresults.govt.nz. Iliwekwa mnamo 2025-10-24.
  11. "Party Lists of Successful Registered Parties". electionresults.govt.nz. Iliwekwa mnamo 2025-10-24.
  12. "NZ Election 2020: Teenagers Luke Wijohn, William Wood on why they're standing for Parliament", Newshub (kwa Kiingereza), 2020-10-08, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-08-29, iliwekwa mnamo 2025-10-24