Taasisi ya Goethe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Makao makuu ya Taasisi ya Goethe mjini Munich

Taasisi ya Goethe (kwa Kijerumani: Goethe-Institut) ni taasisi ya kiutamaduni yenye shabaha ya kufundisha lugha ya Kijerumani na kujenga mawasiliano ya kiutamaduni kote duniani.

Jina na kazi[hariri | hariri chanzo]

Jina la Goethe linamkumbusha mtaalamu na mshairi maarufu Mjerumani Johann Wolfgang von Goethe.

Kazi kuu ya tasisi hiyo ni kufundisha lugha na kueleza utamaduni wa Kijerumani kote duniani. Hii ni pamoja na kueneza filamu, muziki na tamthiliya kutoka Ujerumani, kuwa na maktaba ya vitabu vya Kijerumani, kuwakaribisha wanafunzi wasome Ujerumani, na kufanya warsha za kueleza mawazo yaliyo muhimu katika jamii ya Ujerumani pamoja na mafundisho kuhusu haki za binadamu na demokrasia.

Umbo lake[hariri | hariri chanzo]

Taasisi ya Goethe ina umbo la asasi isiyo ya kiserikali lakini inapokea pesa zake kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, kwa hiyo inaitegemea na kufuata matakwa yake. Pia wanachama wake ni hasa mikono ya serikali za ngazi mbalimbali za Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani yaani wawakilishi wa serikali kuu na serikali za majimbo ya Ujerumani pamoja na wajumbe wa bunge la shirikisho lakini pia wajumbe wengine kutoka pande mbalimbali za maisha ya kiutamaduni ya Ujerumani wasiozidi watu 29.

Vituo[hariri | hariri chanzo]

Taasisi huwa na vituo 13 katika Ujerumani na vingine 136 katika nchi 92. Taasisi ya Goethe inashirikiana pia na taasisi za kienyeji 800 katika nchi mbalimbali ambazo zinafundisha hasa lugha zikishauriwa na kukaguliwa na taasisi ya Goethe.

Katika Afrika ya Mashariki kunaː

  • Goethe-Institut Tanzania, Alykhan Road No. 63, opposite Jamatkhana Moschee, Upanga, Dar es Salaam, simu: +255 22 213 4800, anwani ya barua pepe: info@daressalaam.goethe.org, anwani ya posta: P.O. Box 9541, Dar es Salaam, Tanzania; tovuti: www.goethe.de/tansania
  • Goethe-Institut Nairobi or German Cultural Centre Nairobi, Corner Loita/Monrovia-Street, Maendeleo House, Nairobi, Kenya; anwani ya posta: P.O.B. 4 94 68, 00100 Nairobi GPO/Kenia, phone: +254 20 2224640, fax +254 20 340770, info@nairobi.goethe.org, tovuti: www.goethe.de/nairobi
  • Goethe-Zentrum Kampala, 6 Mackinnon Road, Nakasero, P.O. Box 11778, Kampala, Uganda; Tel. +256 414 533410, Mob. +256 775652312, info@goethezentrumkampala.org, tovuti: www.goethe.de/kampala

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Taasisi ya Goethe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.