T. B. Joshua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Temitope Balogun Joshua (aliyefahamika zaidi kwa jina la T. B. Joshua; 12 Juni 1963 - 5 Juni 2021) alikuwa mchungaji na nabii kutoka nchi ya Nigeria ambaye hujulikana kwa kusaidia watu wenye matatizo kwa njia mbalimbali, yakiwemo maombezi ya papo kwa papo na kwa njia ya televisheni.

Alikuwa mwanzilishi na kiongozi wa Sinagogi na Kanisa la Mataifa yote (The Synagogue, Church Of All Nations)[1][2] ambalo pia ni shirika la Kikristo linaloendesha kituo cha televisheni kiitwacho Emmanuel TV kilichopo katika mji wa Lagos nchini Nigeria.

T. B. Joshua alikuwa na umaarufu barani Afrika na zaidi katika mitandao ya kijamii, akiwa na wafuasi wapatao 2,500,000 katika mtandao wa Facebook[3][4] na takribani wafuasi 500,000 kwenye mtandao wa YouTube [5] huku akielezwa kuwa mhubiri mkubwa wa Injili[6] na mchungaji maarufu zaidi katika mtandao wa YouTube[7]

Pia Emmanuel TV inadaiwa kuwa televisheni ya Kikristo kubwa na ya kwanza barani Afrika.[8]. Emmanuel TV ni chaneli ya Kikristo inayoongoza kwa kuwa na watazamaji wengi wanaojiunga kuitazama katika mtandao wa YouTube, ikiwa na video zenye watazamaji zaidi ya milioni mia tatu.[9][10]

T. B. Joshua alipewa tuzo mbalimbali za heshima kama vile tuzo ya Officer of the Order of the Federal Republic (OFR) ambayo alipewa na Serikali ya Nigeria mwaka 2008[11] na aliwahi kupigwa kura na watu waongeao lugha ya Kiyoruba na kutangazwa na chombo cha habari cha jamii ya Kiyoruba kuwa mtu wa pekee wa karne.[12].

Aliwahi kuandikwa pia na magazeti ya Kiafrika The Africa Report na New African Magazine kuwa mmojawapo kati ya watu hamsini wenye kuvuta hisia za watu (watu wenye ushawishi mkubwa) zaidi barani Afrika. [13][14]

Kwa mujibu wa gazeti maarufu kutoka nchini Marekani liitwalo Forbes, linaloangazia zaidi mambo ya biashara, uwekezaji, teknolojia, ujasiriamali, uongozi na mitindo ya maisha, T. B. Joshua alitajwa kuwa mchungaji wa tatu kwa utajiri nchini Nigeria[15] ingawa jambo hilo lilipingwa haraka na kanisa lake.[16]

Hata hivyo baada ya kifo chake taarifa nyingine zikaja kujulikana zilizopindua kabisa sura yake katika jamii [17].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. https://www.scoan.org/
 2. "Prophet TB Joshua". Scoan.org. Iliwekwa mnamo 2015-07-16. 
 3. "T.B. Joshua Passes Million Milestone On Facebook", Peace FM (Ghana), 2014-05-29. Retrieved on 2017-08-04. Archived from the original on 2014-07-01. 
 4. Adebowale, Segun. "T.B. Joshua Reaches 2 Million Facebook Fans", The Eagle Online (Nigeria), 2016-03-20. 
 5. Njoku, Ihechukwu. "Emmanuel TV Trumps P-Square, Nollywood To Youtube Milestone", Herald (Nigeria), 2016-09-02. 
 6. Palet, Laura. "The Millionaire On God's Payroll", OZY, 2016-09-18. Retrieved on 2017-08-04. Archived from the original on 2017-08-22. 
 7. Oshin, Tope. "TB Joshua Honoured In Peru After Crusade In South America's Largest Stadium", Signal (Nigeria), 2016-09-27. Retrieved on 2017-08-04. Archived from the original on 2017-08-22. 
 8. Mallinson, Harriet. "Bizarre moment pastor is EXORCISED in desperate bid to save his church", Daily Mail (UK), 2016-08-26. 
 9. Bruce, James. "Skewed Stats", WORLD Magazine (USA), 2015-04-15. 
 10. Yenko, Athena. "Malaysian Flight MH370: Prophecy Video Emerges Dated July 28", International Business Times, 2014-03-12. Retrieved on 2017-08-04. Archived from the original on 2014-10-06. 
 11. Umem, James. "Adeboye, TB Joshua Absent At National Awards", Vanguard, 2008-12-23. 
 12. "Awo, Soyinka, TB Joshua listed as Yoruba icons", Nigerian Tribune, 2015-02-20. Retrieved on 2017-08-04. Archived from the original on 2015-02-28. 
 13. "The 50 Most Influential Africans", The Africa Report, 2012-09-30. 
 14. "2012: 100 Most Influential Africans", New African Magazine, 2012-12-26. 
 15. "Pentecostalism in Africa: Of prophets and profits", The Economist, Oct 4, 2014. Retrieved on 3 October 2014. 
 16. Makhaya, Trudi. "Malaysian Flight MH370: Prophecy Video Emerges Dated July 28", ENCA (South Africa), 2014-09-17. Retrieved on 2017-08-04. Archived from the original on 2021-06-08. 
 17. https://nation.africa/kenya/news/gender/the-dark-secrets-of-televangelist-tb-joshua-s-cult-4520122
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.