Sylvia Owori
Sylvia Owori (alizaliwa 1972) ni mbunifu wa mitindo, mjasiriamali na mtumishi wa serikali wa nchini Uganda.[1] Pia ni mwenyekiti na afisa mtendaji mkuu wa Zipa Modeling Agency, kampuni ambayo alianzisha na kuimiliki.
Vile vile ni mtumishi wa umma katika Ofisi ya Rais katika Serikali ya Uganda. Anaripotiwa kuwa mmoja wa watu wenye utajiri zaidi nchini Uganda, nchi ya tatu kwa uchumi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.[2]
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Owori alizaliwa nchini Uganda, ni mmoja wa watoto saba katika familia yao. Alisoma shule ya sekondari Nsambya, huko Kampala, mji mkuu wa Uganda na jiji kubwa zaidi nchini humo. Alisoma elimu ya juu katika chuo cha Newham huko London, na kuhitimu na kufuzu katika fani ya muundo wa mitindo. Pia ana shahada ya awali katika biashara kutoka Chuo Kikuu cha Derby ambapo alihitimu mnamo 2024. [3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Shaw, Jacqueline (2013). "Sylvia Owori Launches 2013 Vintage Collection". Africa Fashion Guide. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-12-08. Iliwekwa mnamo 6 Desemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Bukumunhe, Timothy (9 Aprili 2007). "Who Are The Richest People In Uganda?". New Vision (Kampala) via Cloud-Computing.Tmcnet.com Quoting Thomson Dialog NewsEdge. Iliwekwa mnamo 7 Desemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Rukundo, Eunice (6 Machi 2011). "Sylvia Owori Has Lived Up To Her Promise To Succeed". Daily Monitor (Kampala). Iliwekwa mnamo 6 Desemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)