Nenda kwa yaliyomo

Sviatoslav Shevchuk

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sviatoslav Shevchuk (alizaliwa Stryi, Ukraina, 5 Mei 1970) ni kiongozi wa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraina ambaye amehudumu kama Askofu mkuu kabisa wa Kyiv–Galicia tangu tarehe 25 Machi 2011.

Wakati alipozaliwa, Kanisa lake halikuwa halali chini ya Umoja wa Kisovyeti. Wazazi na babu na bibi zake walikuwa Wakristo wa Kikatoliki na walihusika katika Kanisa la Siri.

Alikumbuka kwamba wakati wa safari ya familia kuelekea mahali patakatifu la Orthodox la Pochaev takriban mwaka 1985, alisali mbele ya picha ya Theotokos, akieleza hamu yake ya kuwa padri.

Miaka michache baadaye, alipoanza masomo ya udaktari katika jiji la Boryslav, alianza kuhudhuria seminari ya siri huko Yaremche, katika milima ya Karpati. [1] [2]

  1. "Consagración episcopal de Mons. Sviatoslav Shevchuk". Aica on line. Iliwekwa mnamo 24 Machi 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "УНІАН: Главою УГКЦ став єпископ Святослав (Шевчук)". Iliwekwa mnamo 24 Machi 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.