Nenda kwa yaliyomo

Svetlana Kulakova

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Svetlana Kulakova
Amezaliwa 13 Desemba 1982 (1982-12-13) (umri 43)
Sarov, Urusi
Nchi Urusi
Mtindo Mtindo wa kawaida
Uzito Uzani wa Kati Mwepesi
Urefu futi 5 inchi 8

Svetlana Kulakova (amezaliwa tarehe 13 Desemba 1982) ni bondia wa zamani wa kulipwa kutoka nchini Urusi na pia bingwa wa ndondi za ridhaa katika mchezo wa mateke "kickboxing ".

Alitwaa taji la muda la dunia la WBA katika daraja la uzito wa juu wa mwanga (super-lightweight) lililokuwa wazi baada ya kumshinda Judy Waguthii kwa uamuzi wa majaji wote katka mji wa Volgograd,nchini Urusi, mnamo 24 Agosti 2013.[1] Kulakova alifanikiwa kulitetea taji hilo kwa ushindi wa pointi dhidi ya Florence Muthoni katika mji wa Barnaul,nchini Urusi, mnamo 15 Novemba 2013.[2]

Mnamo 1 Juni 2014, alichuana na bingwa kamili wa WBA, Ana Laura Esteche, kwenye mji wa Mytishchi,huko nchini Urusi, lakini pambano hilo liliishia kwa sare.[3] Kulakova alishinda taji la dunia la IBO katika uzito wa juu wa mwanga lililokuwa wazi kwa kumshinda Prisca Vicot lililofanyika katika jiji kuu la nchi ya Urusi la Moscow, mnamo 3 Desemba 2016.[4] Alilitetea taji hilo mara moja katika pambano la marudiano dhidi ya Judy Waguthii mnamo 27 Novemba 2017, ambapo alishinda kwa uamuzi wa majaji wengi.[5]

  1. ↑ "KULAKOVA DOMINANT DESPITE CUT". Asian Boxing.
  2. ↑ "Svetlana Kulakova retiene faja interina de las 140 libras". wbaboxing.com.
  3. ↑ "Russia's rising stars of women's boxing". rbth.com.
  4. ↑ "Results December 2016". worldboxingnews.com.
  5. ↑ "Svetlana Kulakova verteidigte IBO Titel gegen Judy Waguthii". boxwelt.com.