Nenda kwa yaliyomo

Suzanne Elise Walsh

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Suzanne Elise Walsh
AmezaliwaSuzanne Elise Walsh
ElimuHudson Valley Community College, Chuo Kikuu cha Cornell,Chuo Kikuu cha Case Western Reserve

Suzanne Elise Walsh (alizaliwa 1968 au 1969[1]) ni msimamizi wa kitaaluma kutoka Marekani anayehudumu kama rais wa 19 wa Bennett College tangu mwaka 2019.

Walsh alipata stashahada ya kati (Associate Degree) katika Sayansi Tumizi kutoka Hudson Valley Community College[2]. Baadaye alipata shahada ya kwanza katika kazi za ustawi wa jamii (Social Work) kutoka Chuo Kikuu cha Cornell.

Aliendelea na masomo ya juu na kukamilisha Shahada ya Uzamili ya Kazi za Jamii (MSW) pamoja na Shahada ya Sheria (JD) katika Chuo Kikuu cha Case Western Reserve.[3]

Katika taaluma yake ya kazi, Walsh amewahi kufanya kazi katika Heinz Endowments. Hadi mwaka 2018, alikuwa naibu mkurugenzi wa elimu ya juu katika Bill & Melinda Gates Foundation. Mwaka huo huo, aliacha kazi katika taasisi hiyo na kuanza kufanya kazi kama mshauri huru, akianzisha kampuni iitwayo Discerning SEWLutions, LLC.

Mnamo mwaka 2019, Walsh alikuwa akiishi Seattle, Marekani. Tarehe 1 Agosti 2019, aliteuliwa kuwa rais wa 19 wa Bennett College, akimrithi rais wa mpito Gwendolyn O'Neal.

Mwaka 2022, alijiunga na bodi ya kitaifa ya ushauri ya Institute for Emerging Issues.

  1. "New Bennett President Suzanne Walsh Optimistic Amid Crisis". The EDU Ledger (kwa American English). 2019-08-08. Iliwekwa mnamo 2026-01-21.
  2. "Office of the President � Bennett College", Bennett College (kwa American English), ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-01-17, iliwekwa mnamo 2026-01-21 {{citation}}: replacement character in |title= at position 25 (help)
  3. "Suzanne Walsh Joins IEI National Advisory Board", Institute for Emerging Issues (kwa American English), 2022-04-05, iliwekwa mnamo 2026-01-21
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Suzanne Elise Walsh kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.