Nenda kwa yaliyomo

Susan Chomba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Susan Chomba ni mwanasayansi na mwanamazingira kutoka nchini Kenya. Yeye ni mkurugenzi katika Taasisi ya Rasilimali Duniani (World Resources Institute).

Chomba alikulia kwenye jamii ya kimaskini katika kaunti ya Kirinyaga.[1] Chomba alilelewa na kukuzwa na bibi yake pekee ambaye alikuwa anafanya Kazi kwa bidii sana. Mama yake Chomba alikuwa akipanda maharage ya kifaransa kwenye ardhi iliyomilikiwa na baba yake wa kambo na alianzisha kilimo cha kushirikiana.[2]

Chomba alipokuwa na miaka tisa, shule ya bweni katika maeneo waliyokuwa wanaishi ilimkataa kutokana na umasikini wake na WA familia yake ndipo akaenda kusomea maeneo ya Magharibi mwa Kenya. Mama yake aliposhindwa kabisa kulipia ada Chomba alirudi Kirinyaga ambapo alisoma shule ya Provincial (Provincial high school). Kila mwanafunzi katika shule hiyo alipewa kipande cha ardhi ili kulima. Chomba alianza kufanya majaribio ya kulima kilimo cha Organic, alipanda na kukuza kabichi ili kuhimili hali ya hewa ya baridi.[2]

Ingawa Chomba alitarajia kusomea Sheria au Kilimo Uchumi, alipangiwa kozi ya Misitu katika chuo kikuu cha Moi.[2] Katika mwaka wake wa Tatu alipokuwa alisoma masomo ya Kilimo Misitu ndipo alipogundua wito wake.[2]

Chomba alijiunga na Kituo cha Utafiti cha Kimataifa cha Kilimo Misitu(International Centre for Research in Agroforestry), ambapo aliongoza "Regreening Africa", program ya nchi nane ya urejeshaji wa ardhi, mpango uliorejesha hekari milioni moja za ardhi iliyoharibika Afrika.[2]

Chomba alikuwa mshiriki wa kundi la kwanza kuhitimu na shahada ya uzamili ya Ulaya katika Misitu Endelevu ya Tropiki kutoka Chuo Kikuu cha Bangor na Chuo Kikuu cha Copenhagen. Alikamilisha kazi na mafunzo ya vitendo akiwa nchini Tanzania.[3] Aliendelea pia kupata Shahada yake ya Uzamivu (PhD) katika utawala wa misitu katika Chuo Kikuu cha Copenhagen.[2][4]

Mnamo mwaka 2021, Chomba alijiunga na Taasisi ya Rasilimali Duniani kama Mkurugenzi wao wa Mazingira Muhimu kwa Afrika, ambapo anaongoza kazi zinazohusu "Misitu, Mifumo ya Chakula na Watu."[5][4] Pia ni balozi wa kimataifa wa Mbio za Zero na Mbio za Ustahimilivu chini ya Mabingwa wa Ngazi ya Juu wa Umoja wa Mataifa wa Hatua za Mabadiliko ya Tabianchi.[4][6]

  • Tuzo ya Uzamili ya Misitu ya Peter Henry, mpokeaji wa kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Bangor
  • 2016: Wanawake 16 Wanaorejesha Dunia, Jukwaa la Mazingira Duniani[4]
  • 2022: Wanawake 25 wanaounda hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi duniani, Greenbiz[7]
  • 2023: Wanawake 100 (BBC), ambayo inaangazia wanawake 100 wenye msukumo na ushawishi kutoka kote ulimwenguni.[1]


  1. 1 2 "BBC 100 Women 2023: Who is on the list this year? - BBC News". News (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2026-02-11.
  2. 1 2 3 4 5 6 Wadekar, Neha (2023-06-21), "'Women bear the biggest brunt of climate change,' says climate scientist Susan Chomba", The Guardian (kwa Kiingereza (Uingereza)), ISSN 0261-3077, iliwekwa mnamo 2026-02-11
  3. ↑ "Bangor Alumna among world's most influential women". Bangor University (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-02-12.
  4. 1 2 3 4 "Susan Chomba | World Resources Institute". www.wri.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-02-12.
  5. ↑ "Susan Chomba". #ThinkLandscape (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-02-12.
  6. ↑ unfccc.int https://unfccc.int/climate-action/engagement/marrakech-partnership-for-global-climate-action/actors/meet-the-champions/work-of-the-climate-high-level-champions. Iliwekwa mnamo 2026-02-12. {{cite web}}: Missing or empty |title= (help)
  7. ↑ Heather Clancy (2022-03-07). "25 more badass women shaping climate action". Trellis (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-02-20.