Sulley Muntari
| Sulley Muntari | |
| Amezaliwa | 27 Agosti 1984 Konongo, Ashanti, Ghana |
|---|---|
| Nchi | Ghana |
| Urefu | 1.79 m |
Suleyman Ali "Sulley" Muntari (alizaliwa 27 Agosti 1984) alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu kutoka nchini Ghana aliyecheza nafasi ya kiungo.[1] Alitumia sehemu kubwa ya kazi yake ya soka nchini Italia, akichezea klabu kama vile Udinese, Inter Milan, na AC Milan.
Akionekana kama mchezaji mwenye kipaji kikubwa tangu akiwa mdogo, Muntari alianza kazi yake ya soka la vijana nchini Ghana akiwa na klabu ya Liberty Professionals kabla ya kujiunga na Udinese ambapo alipanda kutoka timu ya vijana hadi kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza. Alicheza mechi zaidi ya 150 akiwa na Udinese na kufunga mabao 9 kabla ya kuhamia klabu ya nchini Uingereza ya Portsmouth iliyokuwa ikishiriki ligi kuu ya Uingereza. Alidumu kwa msimu mmoja tu na klabu hiyo na alikuwa sehemu ya timu iliyotwaa Kombe la FA mwaka 2007–08.[2]
Kiwango chake katika Ligi Kuu na Kombe la FA kilimfanya asajiliwe na Inter Milan mwaka 2008. Katika kipindi chake akiwa na Inter Milan, aliisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa ya ulaya mwaka 2009–10 na ubingwa wa Serie A katika misimu ya 2008–09 na 2009–10, pamoja na mataji mengine.
Baada ya kuanza kuichezea timu ya taifa ya Ghana mwaka 2002, Muntari alicheza mechi zaidi ya 80 za kimataifa na alichaguliwa katika vikosi vya mashindano mawili ya Kombe la Mataifa ya Afrika na mashindano matatu ya Kombe la Dunia la FIFA. Pia alikuwa mchezaji wa timu ya Ghana ya vijana chini ya miaka 20 iliyoshika nafasi ya pili katika mashindano ya ubingwa wa Vijana wa Afrika na kombe la Dunia la FIFA la vijana chini ya Miaka 20 yote mawili yakifanyika mwaka 2001.
Yeye ni kaka mkubwa wa aliyekuwa mchezaji wa Tambov, Sulley Muniru.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Sulley Muntari" (kwa English). National Football Teams. Iliwekwa mnamo 28 Septemba 2026.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "Sulley Muntari" (kwa English). Soccerbase. Iliwekwa mnamo 28 Septemba 2026.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link)
| Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sulley Muntari kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |