Nenda kwa yaliyomo

Stephen Joseph Reichert

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Stephen Joseph Reichert (alizaliwa 14 Mei 1943) ni askofu mkuu mstaafu wa Kanisa Katoliki.

Alizaliwa Leoville, Kansas, Marekani, na alipewa daraja ya upadre kwa ajili ya shirika la Wakapuchini tarehe 27 Septemba 1969. Tarehe 3 Februari 1995, Reichert aliteuliwa kuwa askofu wa Dayosisi ya Kikatoliki ya Mendi, Papua New Guinea, na alipewa daraja la uaskofu tarehe 7 Mei 1995. Kisha aliteuliwa kuwa askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Kikatoliki la Madang, Papua New Guinea, tarehe 30 Novemba 2010.

Reichert alistaafu baada ya kufikia kikomo cha umri na ombi lake la kustaafu lilikubaliwa tarehe 26 Julai 2019.[1]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.