Stefania Turkewich

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Stefania Turkewich-Lukianovych

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Stefania Turkewich
Amezaliwa 25 aprili 1898
Asili yake Lviv
Amekufa 8 aprili 1977
Aina ya muziki Muziki wa Klasiki
Kazi yake Mpiga piano, Mtaalamu wa Muziki, Mwalimu wa piano

Stefania Turkewich-Lukianovych (25 Aprili 1898 – 8 Aprili 1977) alikuwa mtunzi wa muziki, mpiga piano na mtaalamu wa muziki kutoka Ukraina. Alikuwa mtunzi wa kike wa kwanza wa muziki wa Ukraina[1]. Matungo yake yalipigwa marufuku kwenye Ukraina na mamlaka ya Umoja wa Kisovyeti.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Stefania alizaliwa huko Lviv, uliokuwa mji wa Austria-Hungaria wakati ule lakini sasa uko Ukrainia. Babu yake (Lev Turkevich) na baba yake (Ivan Turkevich) walikuwa makuhani. Mama yake, Sofia Kormoshiv (Кормошів), alikuwa mpiga piano[2]. Familia nzima ilikuwa ya muziki na kila mtu alicheza ala. Stefania alicheza piano, kinubi na kinanda cha matete (harmonium).

Kabla na baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia alisoma piano na nadharia ya muziki kwa wanamuziki kadhaa, hivi karibuni katika Chuo Kikuu na Chuo cha Muziki vya Lviv[2]: 10 . Alitunga kazi yake ya kwanza ya muziki mwaka wa 1919: Liturjia, ambayo ilifanywa mara kadhaa katika Kanisa Kuu la St. George[3]. Mwaka 1921, alisoma katika Chuo Kikuu cha Vienna na Chuo Kikuu cha Muziki na Sanaa ya Maonyesho Vienna, ambapo alihitimu mnamo 1923 na Diploma ya Ualimu[3]. Miaka 1930-1934, alisoma katika Chuo Kikuu cha Charles huko Praha na katika Chuo cha Muziki cha Praha, na hatimaye akapokea udaktari wake wa somo la muziki katika Chuo Kikuu Huru cha Kiukraina. Tasnifu yake ilikuwa juu ya mada ya Hadithi za Kiukraina katika opera za Kirusi. Alikuwa mwanamke wa kwanza wa Kiukraina kupokea Ph.D.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia aliendelea kufanya kazi huko Lviv, kwanza chini ya Sovyeti na kisha chini ya Nazi. Baada ya vita, mnamo 1946, alikimbia wakomunisti na kuhamia Italia, ambapo mume wake wa pili anafanya kazi kwa Waingereza. Baadaye mwaka huo huo, walihamia Uingereza, ambako aliishi hadi kifo chake mwaka wa 1977.

Matungo[hariri | hariri chanzo]

Kazi za Kisimfonia[hariri | hariri chanzo]

 • Simfonia Nr. 1, 1937
 • Simfonia Nr. 2a, 1952
 • Simfonia Nr. 2b, toleo la pili
 • Simfonieta, 1956
 • Michoro Mitatu ya Kisimfonia, 1975
 • Shairi la Kisimfonia "La Vita"
 • Simfonia ya Anga-nje, 1972
 • Suite kwa okestra mbili za ala za nyuzi
 • Fantasia kwa okestra mbili za ala za nyuzi

Baleti[hariri | hariri chanzo]

 • Msichana Wenye Mikono Iliyodhoofika, Bristol, 1957
 • Mkufu
 • Majira ya Kuchipua (Baleti ya watoto), 1934-1935
 • Mavka - Nimfi wa Msitu, 1964-1967, Belfast
 • The Scarecrow, 1976

Opera[hariri | hariri chanzo]

 • Mavka (isiyomalizika) inategemea Wimbo wa Msitu wa Lesia Ukrainka

Opera za watoto[hariri | hariri chanzo]

 • Tsar Okh au Moyo wa Oksana, 1960
 • Ibilisi Kijana
 • Kitalu cha mboga, 1969

Kazi za kwaya[hariri | hariri chanzo]

 • Liturjia, 1919
 • Zaburi kwa Scheptytsky
 • Kabla ya Vita
 • Michoro mitatu
 • Tumbuizo (Ah, hakuna paka) 1946

Muziki wa chumba[hariri | hariri chanzo]

 • Sonata kwa fidla na piano, 1935
 • Kwarteti ya ala za nyuzi, 1960 - 1970
 • Trio ya fidla, viola na chelo, 1960 - 1970
 • Kwinteti ya piano, 1960 - 1970
 • Trio ya ala za pumzi, 1972

Piano[hariri | hariri chanzo]

 • Mabadilifu ya Mada ya Kiukraina, 1932
 • Fantasia. Suite kwa Piano inayotegemea Mada za Kiukraina, 1940
 • Impromptu, 1962
 • Grotesque, 1964
 • Suite ya Mlima, 1966 - 1968
 • Mzunguko wa Nyimbo kwa Watoto, 1936-1946
 • Nyimbo za Krismasi za Kiukraina na Shtchedrivka
 • Habari njema
 • Krismasi na Mchekeshaji, 1971

Matungo mengine[hariri | hariri chanzo]

 • Moyo, kwa mwimbaji mmoja na okestra
 • Lorelei, Msimulizi, Kinanda cha matete na Piano, 1919. Matini ya Lesia Ukrainka
 • Mei, 1912
 • Mada za Nyimbo za Wenyeji
 • Uwanja wa Uhuru - Wimbo kwa piano
 • Wimbo wa Lemky kwa mwimbaji na ala za nyuzi

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. "Ukrainian Art Song Project – Stefania Turkewich". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-22. 
 2. 2.0 2.1 Павлишин, Степанія Стефанівна. Перша українська композиторка: Стефанія Туркевич-Лісовська-Лукіянович, БаК, Lviv 2004.
 3. 3.0 3.1 Роман Кравець. "Українці в Сполученому Королівстві". Інтернет-енциклопедія. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-04-27. Iliwekwa mnamo 2018-08-28.