Starfalls

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ni kipindi cha televisheni ambacho huoneshwa kwenye chaneli ya nickelodeon ambayo inahusu msanii aitwaye Craig aliyehama pamoja na watoto wake Diamond,Phoenix na Bo brooks kutoka sehemu waliyokuwa wanaishi ambayo ilikuwa inaitwa Alley nakwenda kuishi Star falls.Ambapo huko Star falls wataenda kuishi kwenye nyumba ya mama mmoja aitwaye Beth akiwa na mwanaye Sophia.Ambapo huko sophia na Diamond watakuwa marafiki na kwa pamoja watajaribu kuwaunganisha pamoja ili waweze kuwa ndugu.Upande wa pili kwa mdogo wake Bo brooks yeye na rafiki yake Nate wamekuwa wakicheza na babu yao lou.Kwa upande wa phoenix yeye akijaribu kukuza mawazo yake na kuwashirikisha ndugu zake kwa kuwafanya wamsaidie au kuwaonyesha na kuwauliza kama wamependa sanaa aliyoitengeneza au hawajaipenda na ndugu zake mara nyingi wanasemaga ni nzuri ili kumfurahisha kaka yao.Na kwa upande wa wazazi wao ni kwamba Beth anampenda Craig ila anaogopa kumwambia kwamba anampenda na kwa Craig naye hivyohivyo ila mwisho wa siku wanaambiana kwamba wanapendana lakini cha kushangaza ni kwamba baba yake Beth hampendi Craig ila Diamond na Sophie wanafanya mbinu ili wasichukiane kwa hiyo wanamtuma Nate kwenda kuwaingiza kwenye chumba kimoja ambapo humo ndani wanaelewana na kuwa marafiki na mwishowe Craig na Beth wanakubaliana nakupanga tarehe ya kuowana.