Nenda kwa yaliyomo

Stafanie Taylor

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Stafanie Taylor
Taylor in 2020
Taylor in 2020
Alizaliwa 11 Juni 1991 (1991-06-11) (umri 34)
Nchi Visiwa vya Karibian
Kazi yake Mchezaji wa kriketi

Stafanie Roxann Taylor, OD (alizaliwa tarehe 11 Juni 1991) ni mchezaji wa kriketi kutoka Jamaica na aliyewahi kuwa nahodha wa timu ya kriketi ya wanawake ya West Indies. Ameiwakilisha timu hiyo zaidi ya mara 280 tangu alipofanya debut yake mwaka 2008. Akiwa mchezaji wa kupiga mpira kwa mkono wa kulia na mpiga mipira ya off-break, Taylor alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Kriketi wa Wanawake wa ICC wa mwaka 2011, akiwa Mwest Indies wa kwanza kupokea tuzo hiyo. Pia alikuwa mwanamke wa kwanza kufikisha jumla ya mikimbio 1,000 (runs) katika mechi za ODI kwa niaba ya West Indies..[1]

Katika ngazi ya ligi za ndani, anacheza kriketi kwa Jamaica na Guyana Amazon Warriors, na awali aliwahi kuichezea Auckland, Sydney Thunder, Adelaide Strikers, Western Storm, Southern Vipers, Southern Brave, na Trailblazers.[2]

  1. "Hayley Matthews takes over as West Indies captain from Stefanie Taylor". ESPNcricinfo. Iliwekwa mnamo 25 Juni 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Player Profile: Stafanie Taylor". CricketArchive. Iliwekwa mnamo 20 Mei 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Stafanie Taylor kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.