Spika (muziki)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Spika ya muziki (kutoka Kiingereza: Loudspeaker) ni chombo kinachobadilisha kawi za audio zilizo katika mfumo wa elektroniki na kuzifanya ziwe sauti.

Spika zinazotumika siku hizi zilivumbuliwa na Edward Kellog na Chester Rice mwaka 1925.

Spika hufanya kazi kama kipazasauti. Tofauti ni kuwa kipazasauti hubadilisha sauti kuwa audio zilizo kwa mfumo wa kielektroniki ilhali spika nazo hubadilisha kawi hii kuwa sauti.

Kwa kawaida, spika huwekwa katika chumba au kabineti ambayo mara nyingi huwa na umbo la mstatili au mraba. Kabineti ya spika huenda ikatengenezwa kwa plastiki au mbao. Hili huathiri jinsi sauti itakavyokuwa.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Johann Phillip Reis aliweka spika ya kielektroniki kwa simu yake mwaka 1861. Spika hii iliweza kutoa sauti nzuri na wazi iliyosikika vizuri na kueleweka.

Alexander Graham Bell, mzinduzi wa simu ya kwanza aliidhinisha spika ya simu yake mwaka 1876. Hili lilifuatwa na uzinduzi mwingine bora na Ernst Siemens.

Matumizi ya spika leo[hariri | hariri chanzo]

Spika hutumika nyumbani ikiambatanishwa na redio au runinga ili kutoa sauti nzuri ya muziki. Spika pia hupatikana katika magari.

Kwenye sherehe, mikutano au kwenye mihadhara, spika huambatanishwa na kipazasauti ili anayeongea aweze kufikia watu wote na ujumbe wake uwapate.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Tazama spika kwa maelezo kuhusu mkubwa wa bunge anayeendesha mijadala.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]