Nenda kwa yaliyomo

Sonallah Ibrahim

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Son'allah Ibrahim (19372025) alikuwa mwandishi wa riwaya na hadithi fupi kutoka Misri, na mmoja wa kizazi cha waandishi wa miaka ya 1960 maarufu kwa misimamo yao ya mrengo wa kushoto, ambayo aliionyesha moja kwa moja katika kazi zake.

Riwaya zake, zinajumuisha vipande vingi kutoka magazeti, majarida na vyanzo vingine vya kisiasa ili kuwaelimisha watu kuhusu masuala fulani ya kisiasa au kijamii.

Kutokana na maoni yake ya kisiasa, alifungwa gerezani katika miaka ya 1960; kifungo hicho kimeelezwa katika kitabu chake cha kwanza That Smell (Tilk al-Rā’iha – “Harufu Hiyo”)[1][2]

  1. "Renowned Egyptian novelist Sonallah Ibrahim dies at 88". France 24 (kwa Kiingereza). 2025-08-13. Iliwekwa mnamo 2025-08-13.
  2. Ewa Machut-Mendecka (2007). "Literature-Untamed element (A proposal of a typology of the modern Arabic prose)". Studia Arabistyczne i Islamistyczne. 13: 51. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Januari 2021.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sonallah Ibrahim kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.