Somalia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Somalia
Hii ramani ya mwaka 2002 yanaonyesha maeneo ya Somalia.

Somalia, (kwa Kisomali: Soomaaliya; kwa Kiarabu: الصومال, As-Suumaal), ambayo inajulikana rasmi kama Jamhuri ya Shirikisho ya Somalia, ni nchi kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki katika Pembe ya Afrika.

Kijiografia, imezungukwa upande wa kaskazini-mashariki na Ethiopia na Jibuti, na upande wa magharibi ya kati na Kenya; Ghuba ya Aden nayo iko mashariki.

Mji mkuu na mji mkubwa zaidi ni Mogadishu (wakazi 2,120,000).

Jiografia

Historia

Bosaso, Somalia.

Nchi iliunganika mwaka 1960, kutokana na makoloni mawiliː la Waitalia (kusini) na la Waingereza (kaskazini).

Baada ya mwaka 1991 nchi ya Somalia ilibaki haina serikali wala umoja wa taifa, iligawiwa na wakereketwa na wanamgambo wa ukoo na eneo, hasa Somaliland, Puntland na Galmudug upande wa kaskazini.

Katika miaka 2008-2013 ilihesabika kama nchi filisika. Kwa sasa ni nchi dhaifu lakini inaanza kujengwa upya kama shirikisho.

Watu

Tazama pia: Orodha ya lugha za Somalia

Hii ramani ya mwaka 2002 inaonyesha msongamano wa watu.

Watu asili wa Somalia ni Wasomali (85%) wa makabila ya:

Wengine (15%) ni:

Kisomali ndiyo lugha ya kawaida ya wakazi wengi na lugha rasmi pamoja na Kiarabu. Kati ya lugha nyingine zinazotumika nchini, mojawapo ni Kiswahili.

Upande wa dini, 99.8% ni Waislamu, hasa Wasuni.

Utawala

Tazama pia: Wilaya za Somalia

Maeneo (umoja: gobolka, wingi: gobollada) ya Somalia, ambayo imegawiwa tena kwa wilaya, ni:

  1. Awdal
  2. Bakool
  3. Banaadir
  4. Bari
  5. Bandari
  6. Galguduud
  7. Gedo
  8. Hiiraan
  9. Jubbada Dhexe
  1. Jubbada Hoose
  2. Mudug
  3. Nugaal
  4. Sanaag
  5. Shabeellaha Dhexe
  6. Shabeellaha Hoose
  7. Sool
  8. Togdheer
  9. Woqooyi Galbeed

Utamaduni

Tazama pia: Utamaduni wa Somalia

Uchumi

Tazama pia: Uchumi wa Somalia

Banda la biashara huko Mogadishu.

Mawasiliano

Mawasiliano ya Jamhuri ya Somalia ilikaribia kuangamia kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, lakini kwa sasa kampuni za binafsi za mawasiliano ya mitambo, zimetwaa karibu miji yote Somalia, na hata kutoa huduma njema kuliko nchi zilizo jirani.

Somalia ni nchi mojawapo Afrika ambayo ina mawasiliano ya bei rahisi zaidi, pengine kwa kuwa Somalia haikuwa na serikali iliyotoza ushuru; (Telecoms thriving in lawless Somalia) Kampuni zinazohudumia watu wa Somalia ni kama:

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Habari, mitandao inayojadili kuhusu Somalia.
Habari za kawaida
Watambuzi


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Somalia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.