Mngogwe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Solanum macrocarpon)
Mngogwe
(Solanum aethiopicum na S. macrocarpon)
Mngogwe wa Afrika
Mngogwe wa Afrika
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Asterids (Mimea kama alizeti)
Oda: Solanales (Mimea kama mnavu)
Familia: Solanaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mnavu)
Jenasi: Solanum
L.
Spishi: S. aethiopicum L.

S. macrocarpon L.

Mngogwe au mnyanya-chungu ni jina la spishi mbili za jenasi Solanum katika familia Solanaceae.

Matunda yake huitwa ngogwe na huliwa baada ya kupikwa, ila ngogwe Uhabeshi huliwa mbichi pia.

Majani yaliyopikwa huliwa vilevile na huitwa mafa.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Asili ya mngogwe wa Afrika ni Afrika ya Magharibi na asili ya mngogwe Habeshi ni Uhabeshi, lakini siku hizi spishi zote mbili hukuzwa mahali pengi pa Afrika na katika Asia na Amerika pia.

Mngogwe Habeshi hupendwa sana katika Afrika ya Magharibi. Waigbo wa Nijeria wanatumia matunda yake kama mbadala wa koko ya kola.

Picha[hariri | hariri chanzo]