Nenda kwa yaliyomo

Sofia Boutella

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sofia Boutella (kwa Kiarabu: صوفيا بوتلة; alizaliwa 3 Aprili 1982)[1] ni mwigizaji, mchezaji wa ngoma na mwanamitindo [2]wa asili ya Algeria na Ufaransa. Alizaliwa mjini Algiers, Algeria, kisha alihamia Paris akiwa na umri wa miaka 10.

Baada ya muda mfupi, alianza mazoezi ya michezo ya sarakasi ya mdundo na aliingia kwenye timu ya taifa ya Ufaransa akiwa na umri wa miaka 18.[3]

Alianza kucheza ngoma kwenye filamu, vipindi vya televisheni, matangazo ya biashara na tamasha za muziki[4]. Alikuwa mmoja wa wachezaji wa nyuma wa mwimbaji Madonna kwa miaka sita, akicheza kwenye video nyingi za muziki na pia kwenye tamasha la Super Bowl la mwaka 2012.

Kama mwigizaji, alipata mafanikio makubwa mwaka 2012 alipocheza filamu ya Uingereza iitwayo StreetDance2.[5]

  1. "On This Day in History - April 3rd - Almanac - UPI.com". UPI (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-02-02.
  2. AlloCine, Sofia Boutella (kwa Kifaransa), iliwekwa mnamo 2026-02-02
  3. Clay Skipper (2017-12-05). "Sofia Boutella Is the Best New Action Star of 2017". GQ (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-02-02.
  4. Krista Smith (2017-06-07). "Introducing Sofia Boutella, Your Newest Mummy". Vanity Fair (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-02-02.
  5. "La Momie: Sofia Boutella, une danseuse franco-algérienne adoptée par Hollywood". L'Express (kwa Kifaransa). 2017-06-14. Iliwekwa mnamo 2026-02-02.