Slick Rick
Slick Rick | |
---|---|
![]() Slick Rick akitumbuiza mnamo 2009 | |
Amezaliwa | Richard Martin Lloyd Walters Januari 14 1965 |
Majina mengine | |
Uraia |
|
Kazi yake | |
Miaka ya kazi | 1984–hadi sasa |
Ndoa | Mandy Aragones (m. 1997–present) |
Watoto | 2 |
Musical career | |
Studio | |
Richard Martin Lloyd Walters[1] (amezaliwa 14 Januari 1965[2]) ni rapa, mwandishi wa nyimbo, na mtayarishaji wa muziki mwenye asili ya [Uingereza]] lakini aliyejulikana zaidi nchini Marekani. Anajulikana zaidi kwa jina lake la kisanii kama Slick Rick. Mmoja kati ya wanakundi la Doug E. Fresh & the Get Fresh Crew katika miaka ya 1980. Slick ni huhesabiwa kuwa mmoja wa marapa bora wa enzi ya kizazi cha dhahabu cha hip hop kutokana na ujuzi wake wa kusimulia hadithi kupitia muziki wake.
Mnamo mwaka wa 1986, Slick Rick alikuwa msanii wa tatu kusaini mkataba na Def Jam Recordings. Ameachia albamu nne chini ya lebo hiyo: The Great Adventures of Slick Rick (1988), The Ruler's Back (1991), Behind Bars (1994) na The Art of Storytelling (1999). Muziki wake umetumika kama sampuli kwa mara zaidi ya 1,000, katika nyimbo za wasanii akiwemo Eminem, Beyoncé, Mariah Carey, Beastie Boys, TLC, Nas, Miley Cyrus, Kanye West, MF DOOM, Czarface, Black Star, The Notorious B.I.G., Snoop Dogg, MC Ren, Montell Jordan, Tech N9ne, Lloyd, na Color Me Badd.[3]
Katika mchakato huo, Slick Rick amekuwa mmoja wa wasanii wa hip-hop waliosampuliwa zaidi katika historia. Nyimbo nyingi zinazotokana na sampuli za Slick Rick zimekuwa bab-kubwa. Alikuwa mmoja wa wasanii wa kwanza wa hip-hop kufunikwa, wakati Snoop Dogg (wakati huo Snoop Doggy Dogg) alipoimba mistari ya Rick kutoka kwenye rekodi yake "La Di Da Di" karibu yote kwenye wimbo "Lodi Dodi" kwenye albamu yake ya kwanza Doggystyle mwaka 1993.[4] Wakati huo, haikuwa kawaida kwa wanamuziki wa rap kurekodi (kurudia) nyimbo za wasanii wenza wa hip hip.[5][6]
Slick Rick ameshimishwa na VH1 Hip Hop Honors, na About.com ilimuorodhesha namba 12 kwenye orodha yao ya MCs 50 Bora wa Wakati Wetu[7], wakati The Source ilimorodhesha namba 15 kwenye orodha yao ya Waimbaji 50 Bora wa Wakati Wote.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Slick Rick alizaliwa mjini London, Uingereza, lakini familia yake ilihamia katika Bronx, New York, Marekani, alipokuwa mdogo. Alizaliwa na tatizo la macho ambalo lilisababisha kuvaa kiraka cha jicho, ambacho baadaye kilikuwa sehemu ya muonekano wake wa kipekee katika hip hop.
Kazi ya muziki
[hariri | hariri chanzo]Slick Rick alianza kujulikana katika tasnia ya hip hop kupitia kundi la Get Fresh Crew akiwa na Doug E. Fresh. Mnamo mwaka 1985, alishirikiana katika nyimbo mbili maarufu, "The Show" na "La Di Da Di," ambazo zilipata umaarufu mkubwa na kuwa kati ya nyimbo zinazoheshimiwa sana katika historia ya hip hop.
Mwaka 1988, alitoa albamu yake ya kwanza, The Great Adventures of Slick Rick, ambayo ilijumuisha nyimbo maarufu kama "Children's Story," "Hey Young World," na "Teenage Love." Albamu hii ilifanikiwa sana na kumpa nafasi kama mmoja wa waandishi wa hip hop bora wa wakati wake.
Baadaye, Slick Rick alikumbwa na matatizo ya kisheria yaliyopelekea kufungwa gerezani kwa muda, lakini alirejea kwenye muziki na kuendelea kutoa albamu kama The Ruler's Back (1991), Behind Bars (1994), na The Art of Storytelling (1999). Albamu yake ya mwisho ilipata mapokezi mazuri na kuthibitisha kuwa bado alikuwa na uwezo mkubwa wa kisanii.
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]- The Great Adventures of Slick Rick (1988)
- The Ruler's Back (1991)
- Behind Bars (1994)
- The Art of Storytelling (1999)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "The 30 Biggest Criminal Trials in Rap History". Complex (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-02-10.
- ↑ cleveland com Mike Rose (2023-01-14). "Today's famous birthdays list for January 14, 2023 includes celebrities Dave Grohl, Carl Weathers". cleveland (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-02-10.
- ↑ Driscoll, Michael (2019-05-22), "How 'La Di Da Di,' a B-Side From 1985, Became One of Music's Most-Sampled Songs", Wall Street Journal (kwa American English), ISSN 0099-9660, iliwekwa mnamo 2025-02-10
- ↑ HipHopDX- https://hiphopdx.com (2014-07-18). "Dana Dane Says Snoop Dogg's "La-Di-Da-Di" Cover Completely Changed Rap". HipHopDX (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-02-10.
{{cite web}}
: External link in
(help)|author=
- ↑ "Top 10 All Time Most Sampled Records in Hip Hop – WhoSampled.com Blog". web.archive.org. 2016-04-20. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-04-20. Iliwekwa mnamo 2025-02-10.
{{cite web}}
: CS1 maint: bot: original URL status unknown (link) - ↑ "Top 10 Most Sampled Songs Of All Time - PixelVulture". web.archive.org. 2017-08-09. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-08-09. Iliwekwa mnamo 2025-02-10.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-12-31. Iliwekwa mnamo 2025-02-10.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Wasifu wa Slick Rick kwenye AllMusic
Wasifu wa Slick Rick kwenye IMDb
![]() |
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Slick Rick kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |