Nenda kwa yaliyomo

Sirin bint Shamun

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sirin bint Shamun (kwa Kiarabu: سيرين بنت شمعون) alikuwa suria Mkristo Mkopti kutoka Misri, aliyetumwa pamoja na dada yAke Maria al-Qibtiyya kama zawadi kwa nabii wa Kiislamu Muhammad na afisa wa Misri Muqawqis mwaka 628.

Kulingana na mwanahistoria Ibn Saad, ndugu wote wawili walisilimu walipokuwa njiani kuelekea Arabia kwa kushawishiwa na Hatib ibn Abi Balta'ah, ambaye alikuwa ametumwa kama mjumbe kwa gavana wa Misri. [1]

Sirin aliolewa na mshairi Hassan ibn Thabit, akamzalia mtoto wa kiume, Abdurahman ibn Hassan. [2]

  1. Hidayatullah, Aysha (2010). "Māriyya the Copt: gender, sex and heritage in the legacy of Muhammad's umm walad". Islam and Christian–Muslim Relations. 21 (3): 221–243. doi:10.1080/09596410.2010.500475. ISSN 0959-6410. S2CID 145060435.
  2. Tabari, p. 131.