Sinbad (mchekeshaji)
Sinbad | |
![]() Sinbad mnamo 2008 | |
Amezaliwa | 10 Novemba 1956 Benton Harbor, Michigan, Marekani |
---|---|
Nchi | Marekani |
Majina mengine | David Adkins |
Kazi yake | Mchekeshaji, mwigizaji |
Sinbad (alizaliwa kama David Adkins mnamo 10 Novemba 1956) ni mchekeshaji na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Alipata umaarufu katika miaka ya 1990 kupitia vipindi vyake vya HBO, na pia kwa kuonekana kwenye mfululizo wa televisheni kama A Different World (1987–1991) na The Sinbad Show (1993–1994). Ameigiza katika filamu kadhaa, zikiwemo Houseguest (1995), Jingle All the Way (1996), na Good Burger (1997) . Baada ya kusimama kazi kwa kutokana na kuumwa kiharusi, mwaka wa 2025 alirejea kama Benny katika filamu ya Tyler Perry, Straw.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Sinbad alizaliwa Benton Harbor, Michigan, akiwa mtoto wa Louise na Donald Beckley Adkins Sr., mchungaji wa Baptist. Alisoma katika Chuo Kikuu cha Denver, ambako alicheza mpira wa kikapu kabla ya kuanza safari yake ya ucheshi .
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Sinbad alianza kama mchekeshaji wa kusimama na alishiriki katika shindano la Star Search, ambako alifika fainali. Baadaye alionekana katika kipindi cha The Redd Foxx Show kabla ya kupata nafasi kubwa katika A Different World .
Filamu na televisheni
[hariri | hariri chanzo]Sinbad ameonekana katika filamu na vipindi vya televisheni kadhaa, akijulikana kwa mtindo wake wa ucheshi safi na wa familia. Baadhi ya filamu zake maarufu ni:
- Houseguest (1995)
- Jingle All the Way (1996)
- Good Burger (1997) .
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Sinbad alifunga ndoa na Meredith Adkins mwaka 1985, wakatalikiana mwaka 1992, kisha wakaoana tena mwaka 2002. Wana watoto wawili, Paige Adkins na Royce Beckly Adkins .
Filmografia
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Jina la Filamu | Uhusika |
---|---|---|
1989 | That's Adequate | Mchezaji wa mpira |
1993 | Coneheads | Otto |
1995 | Houseguest | Kevin Franklin |
1996 | Jingle All the Way | Myron Larabee |
1996 | First Kid | Sam Simms |
1997 | Good Burger | Mr. Wheat |
2002 | Crazy as Hell | Mgonjwa wa akili |
2013 | Planes | Roper (sauti) |
2025 | Straw | Benny |
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Sinbad at the Internet Movie Database