Simon West
| Simon West | |
| Amezaliwa | 17 Julai 1961 Letchworth, Hertfordshire, Uingereza |
|---|---|
| Nchi | Uingereza |
| Majina mengine | Simon Alexander West |
| Kazi yake | Mwongozaji wa filamu, Mtayarishaji wa filamu |
| Anajulikana kwa ajili ya | Kuongoza filamu kama Con Air, Lara Croft: Tomb Raider, The Mechanic, The Expendables 2 |
Simon Alexander West (amezaliwa tarehe 17 Julai 1961)[1] ni mtayarishaji na mwongozaji wa filamu kutoka Uingereza. Amejikita zaidi katika aina ya filamu za mapigano, hasa kama mwongozaji wa filamu Con Air, Lara Croft: Tomb Raider, The Mechanic, na The Expendables 2. Nje ya filamu za mapigano, kadhalika ameongoza filamu kama The General's Daughter na When a Stranger Calls. Kabla ya kuanza kazi yake ya filamu, West alikuwa muongozaji wa video za muziki kama "Never Gonna Give You Up" ya Rick Astley.[2]
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]West alizaliwa katika Letchworth, Hertfordshire. Alianza kazi yake kama mhariri msaidizi wa filamu kwenye Idara ya Filamu ya BBC, ambapo alifanya kazi katika tamthilia na filamu za hali halisi (makala). Kisha aliacha kazi BBC ili kuingia kwenye matangazo ya biashara na video za muziki. Binti yake, Lillie West, ambaye ni mwanamuziki wa bendi ya Lala Lala, alielezea uzoefu wake wa kuwa mtoto wa mtayarishaji wa filamu katika mahojiano na Paper Magazine mwaka 2018:
"Baba yangu ni mtayarishaji wa filamu, na amerekodi karibu kila tukio la maisha yangu tangu kuzaliwa kwangu."[3]
Filmografia
[hariri | hariri chanzo]Filamu
[hariri | hariri chanzo]Mwelekezaji
| Mwaka | Jina | Maelezo |
|---|---|---|
| 1997 | Con Air | |
| 1999 | The General's Daughter | |
| 2001 | Lara Croft: Tomb Raider | Pia mwandishi |
| 2006 | When a Stranger Calls | |
| 2011 | The Mechanic | |
| 2012 | The Expendables 2 | |
| Stolen | ||
| 2015 | Wild Card | |
| 2016 | Gun Shy | |
| 2017 | Stratton | |
| 2019 | Skyfire | |
| 2024 | Old Guy | |
| 2025 | The Legend Hunters | Iliyoongozwa pamoja na Li Yifan |
| Bride Hard |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Index entry". FreeBMD. ONS. Iliwekwa mnamo 22 Septemba 2021.
- ↑ "Director Simon West: From Rick Astley to Con Air to Skyfire (Interview)". AMFM Magazine.tv (kwa American English). 2021-01-18. Iliwekwa mnamo 2022-03-21.
- ↑ www.papermag.com