Nenda kwa yaliyomo

Sikukuu za Ethiopia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sikukuu za Ethiopia zinafanyika katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, katika Pembe ya Afrika inayopakana na Sudan Kusini, Kenya, Eritrea, Jibuti, na Somalia. Ethiopia ni nchi ya pili kwa wingi wa watu barani Afrika, hivyo utamaduni wake ni wa aina mbalimbali, ukiwa na mila tofauti za kitamaduni. Mazoea ya kitamaduni hutofautiana na ni maalumu kulingana na eneo, dini, na kabila. Kwa sababu hii, watu wa Ethiopia, kama ilivyo katika nchi nyingi ulimwenguni, husherehekea misimu ya sikukuu, lakini Ethiopia ina mila zake za kipekee na zenye mvuto wa pekee.

Watu wengi nchini Ethiopia ni Wakristo wa dhehebu la Kiorthodoksi. Krismasi katika Ethiopia inaitwa “Genna.” Genna ni tarehe muhimu katika kalenda ya Kiorthodoksi ya Ethiopia. Nchini Ethiopia, watu husherehekea Krismasi tarehe saba ya mwezi wa kwanza kwa sababu Ethiopia inafuata kalenda ya Julian, ambayo ina Krismasi tarehe hiyo.

Kalenda ya Ethiopia huanza tarehe 11 mwezi wa tisa na ina miezi kumi na mitatu. Miezi kumi na miwili ina siku thelathini kila moja. Mwezi wa kumi na tatu una siku tano, au sita katika mwaka mrefu (leap year).[1]

Genna ni sherehe ya msimu ya kutafakari kiroho. Kabla ya sikukuu, watu huanza na kipindi cha mfungo kinachoitwa Tsome Nebiyat au mfungo wa manabii. Wakati wa mfungo, watu hawali  nyama wala kunywa pombe. Asubuhi ya Krismasi, watu huenda kanisani. Baada ya ibada, watu hucheza dansi na mchezo wa kitamaduni uitwao Yagenna Chewata. Pia, watu hufungua saumu kwa kula doro wat (mchuzi wa kuku), mayai ya kuchemsha, na injera (aina ya chapati laini ya nafaka). [2]

Watu huvaa nguo nyeupe za kitamaduni zilizotengenezwa kwa kitambaa cheupe chenye mistari myeupe inayong’aa, kinachoitwa netela. Mara kwa mara, watu hupeana zawadi.[3]

Enkutatash

[hariri | hariri chanzo]
Watu wanasherehekea Enkutatash

Enkutatash ni Mwaka Mpya wa Ethiopia, unaosherehekewa tarehe 11 ya mwezi wa tisa. Jina “Enkutatash” linahusishwa na zawadi za vito, na kuna imani kuwa linaanzia na hadithi ya Malkia wa Sheba aliyerejea Ethiopia zaidi ya miaka elfu tatu iliyopita. Kurudi kwa Malkia wa Sheba kunawakilisha mwisho wa ukame wa muda mrefu na mwanzo wa maisha mapya nchini.

Sikukuu hii husherehekewa kwa kutoa zawadi na maua ya njano. Wanawake huimba nyimbo za kitamaduni. Watu hula doro wat na injera, na hunywa divai ya asali pamoja na kahawa. Usiku, familia huwasha choto na kusherehekea hadi alfajiri.[4]

Irreechaa

[hariri | hariri chanzo]
Watu wanasherehekea Enkutatash

Irreechaa ni sherehe ya shukrani kwa watu wa kabila la Oromo, moja ya makabila makubwa nchini Ethiopia. Irreechaa husherehekewa kila mwaka mwezi wa tisa, kama ishara ya kushukuru kwa uzazi na maisha waliyopewa na Mungu wao aitwaye Waaqa.

Irreechaa huadhimishwa wakati wa mwanzo wa majira ya machipuo, baada ya kipindi cha mvua na giza la majira ya baridi. Watu husafiri hadi mtoni au mlimani wakiwa wamevaa mavazi ya kitamaduni ya Oromo, kucheza dansi barabarani, kuimba nyimbo, na kuweka maua mtoni kama ishara ya shukrani.[5]

  1. "Ethiopian Holidays 2025, Ethiopia Holidays Calendar 2017". Ethiopian Calendar (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-04-25.
  2. "Genna, the Ethiopian Christmas". Reino de Aksum (kwa Kihispania). 2024-01-06. Iliwekwa mnamo 2025-04-25.
  3. "Celebrating Ganna: An Ethiopian Tradition". Expedition Subsahara (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-04-25.
  4. "Ethiopian New Year | Brilliant Ethiopia". www.brilliant-ethiopia.com (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2025-04-25.
  5. "What is Irreechaa?". Advocacy for Oromia (kwa Kiingereza). 2022-07-02. Iliwekwa mnamo 2025-04-25.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]